Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Mei 2020 19:01:39
Azithromycin
Azithromycin yenye jina jingine la Zithromax, ni dawa jamii ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria iliyo kwenye kundi la macrolide. Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge, tembe na kimiminika kwa ajili ya kunywa au kimininika kwa ajili ya kutumika kwa kuchoma sindano.
Fomu ya dawa
Hupatikana kwenye fomu ya Tembe yenye uzito wa miligramu 250 au 500
Ufyonzwaji wa Azithromycin
Mara baada ya kunywa kidonge chenye miligramu 250, asilimia 38 tu ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye mzunguko wa damu.
Utoaji wa mabaki ya Azithromycin
Nusu maisha ya dawa ni masaa 68, dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na kinyesi
Mwingiliano wa Azithromycin na dawa zingine
Kutumia dawa hii pamoja na Efavirenz au fluconazole huleta mwingiliano wa wastani. Dawa ya nelfinavir huongeza kiwango cha dawa hii kwenye damu.
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Azithromycin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja nadawa zifuatazo;
Warfarin
Venetoclax
Vemurafenib
Vandetanib
Umeclidinium bromide/vilanterol
Toremifene
Topotecan
Saquinavir
Riociguat
Rimegepant
Protamine
Pomalidomide
Pimozide
Phenindione
Panobinostat
Ondansetron
Macimorelin
Lefamulin
Inotuzumab
Hydroxychloroquine sulfate
Heparin
Glasdegib
Fondaparinux
Enoxaparin
Dronedarone
Digoxin
Dalteparin
Colchicine
Cobicistat
Cisapride
Cholera vaccine
Chanjo hai ya bcg
Bivalirudin
Bemiparin
Arsenic trioxide
Argatroban
Antithrombin III
Antithrombin alfa
Namna Azithromycin inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia kutengenezwa kwa vijenzi muhimu vya bakteria. Hufanya hivyo kwa kupinga utendaji kazi wa vinasaba vya bakteria.
Bakteria wanashambuliwa na azithromycin
Dawa hii hutumika kwenye matibabu yaliyoosababishwa na bakteria wafuatao’
Bakteria Gram-positive
Staphylococcus aureus
Streptococcus agalactiae
Streptococcus pneumoniae
Streptococcus pyogenes
Beta-hemolytic streptococci (Groups C, F, G)
Viridans group streptococci
Bakteria gram-negative
Haemophilus ducreyi
Haemophilus influenzae
Moraxella catarrhalis
Neisseria gonorrhoeae
Bordetella pertussis
Bakteria wa anaerobiki
Peptostreptococcus species
Prevotella bivia
Bakteria wengine
Chlamydophila pneumoniae
Chlamydia trachomatis
Mycoplasma pneumonia
Ureaplasma urealyticum
Legionella pneumophila
Magonjwa yanayotibiwa na Azithromycin
Maambukizi ya muda mfupi ya bakteria kwa wagonjwa wa COPD
Maambukizi ya muda mfupi ya sinusaitizi iliyosababishwa na bakteria
Nimonia ya jamii
Pharynjaitis/tonsilaitizi
Maambukizi ya ngozi yasiyo sugu
Urethritizi and servisaitizi
Vidonda sehemu za siri kutokana na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende
Tafiti mpya za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa Azithromycin inaweza kuzuia uzalianaji wa virusi vinavyosababisha COVID-19. Soma zaidi katika makala ndani ya tovuti hii inayohusu dawa za kutibu COVID-19 kupata maelezo zaidi kuhusu namna dawa hii inavyofanya kazi kwenye matibabu ya COVID-19
Wakati gani usitumie dawa ya Azithromycin
Una mzio na dawa hii au dawa zingine jamii ya macrolide au ketolide pia kama uliwahi pata manjano ya cholestatiki
Tahadhari
Husababisha mzio
Huongeza muda wa QT kwenye moyo
Huwa sumu kwenye ini- endapo dalili za hepataitiz zinatokea acha mara moja kuendelea na dozi ya dawa hii. Dalili ni manjano, kuferi kwa ini na nekrosisi kwenye ini.
Tumia kwenye matibabu ya nimonia iliyosababishwa na bakteria aina ya Chlamydia pneumoniae, Haemophilus influenzae, Mycoplasma pneumoniae au Streptococcus pneumonia
Hupelekea kuharisha kutokana na maambukizi ya clostridium deficile
Taarifa muhimu kwa mgonjwa kuhusu Azithromycin
Dawa hii inaweza kutumiwa pamoja au pasipo chakula. Unapotumia dawa hii hakikisha hautumii sambamba na dawa za kupunguza uzalishaji tindikali jamii ya aluminium na magneziamu.
Matumizi ya Azithromycin kipindi cha ujauzito na kundi lake kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi wakati wa ujauzito
Hakuna tafiti za kutosha kuhusu madhara wakati wa ujauzito kwa kichanga. Itumike kwa tahadhari endapo inahitajika.
Kwa mama anayenyonyesha
Haifahamiki kama dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama au la. Kwa sababu dawa nyingi huingia kwenye maziwa ya mama, tahadhari inatakiwa kuchukuliwa endapo dawa hii itatumika kwa mama anayenyonyesha
Maudhi ya Azithromycin
Kuhisi mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Maumivu ya kifua
Tumbo kujaa gesi\kujamba
Kutapika
Choo cheusi
Manjano ya kolestatiki
Miwasho ukeni
Nefraitizi
Maumivu ya kichwa, kizunguzungu
Kuhisi vitu vinazunguka
Huzuniko
Uchovu
Harara kwenye ngozi
Kuongezeka hisia za macho kwenye mwanga na
Angioidima
Ufanye nini endapo umesahau dozi yako ya Azithromycin?
Endapo umesahau kunywa dozi yako, kunywa mra pale utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi umekaribia sana, acha na kunywa dozi inayofuata. Usinywe dozi mbili kwa wakati mmoja.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-