Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Mei 2020, 04:59:21

Bosentan
Bosentan ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu kwenye mishipa ya palimonari iliyopo kwenye kundi la Endothelin Receptor Antagonisti. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Tracleer.
Rangi ya dawa hii ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.
Bosentan inaweza kumezwa pamoja au pasipo chakula mara mbili kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na Daktari.
Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa .Dozi utakayopewa itategemea hali yako ya kiafya na jinsi mwili unavyokubali matibabu.
Bosentan hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;
• 62.5mg
• 125 mg
Namna dawa inavyofanya kazi;
• Dawa hii hupinga ufanyaji kazi wa homoni ya Endothelian 1 ambayo hufanya kazi ya kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu na kuongeza shinikizo la damu. Homoni hii hupitia kwenye risepta za Endothelian A na B ili kuleta madhara yake ya kuongeza shinikizo la damu. Dawa ya bosentan inapopiga ufanyaji kazi wa homoni endothelin-1 hupelekea kupungua kwa shinikizo la damu kwenyte mishipa ya palmonari.
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la Endothelin Receptor Antagonist) na dawa hii ni;
• Sitaxentan
• Ambrisentan
• Atrasentan
• Zibotentan
• Macitentan
• Tezosentan
Kazi ya dawa :
• Hutumika kushusha shinikizo la damu la juu kwenye mishipa ya ateri ya palmonari.
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la Endothelin Receptor Antagonisti
• Husaidia kupunguza kiasi cha vidonda hasa kwenye vidole kwa watu wenye ugonjwa wa Scleroderma.
Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;
• Esketamine ya kupaka ndani ya pua
• Lemborexant
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aminotransferase ya juu hawapaswi kutumia dawa hii.
Tahadhari ya dawa hii
Hupelekea sumu kwenye ini.
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi X la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Tafiti za wanyama na binadamu zimethibitisha kutokea kwa ulemavu kwa kichanga atakayezaliwa na zipo hatari nyingi za dawa hii hivyo haipaswi kutumika kwa mama mjamzito. Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu huingia kwenye maziwa ya mama.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
• Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji
• Kichwa kuuma
• Haipotension
• Maumivu ya misuli
• Palpitation
• Upungufu wa damu
• Pua kubana
Mengine yanayofanyika Mwilini
Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 3 hadi 5 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 5. Dawa hii hutolewa mwilini kupitia nyongo na hutolewa kidogo kwa njia ya mkojo kwa asilimia 3.
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-