Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Mei 2020, 21:28:33
Cimetidine
Cimetidine ni dawa ambayo inazuia kutolewa kwa histamine na hivyo kuzuia kutengezwa kwa tindikali tumboni. Hivyo dawa hii hutumika kutibu matatizo mbalimbali yanayotokana na tindikali ya tumboni.
Majina mengine
Tagamet
Eureceptor
Tametin
Dyspamet
Ulcedine
Fomula ya kikemikali
C10H16N6S
Jina la kisayansi (IUPAC)
1-cyano-2-methyl-3-[2-[(5-methyl-1H-imidazol-4-yl) methylsulfanyl] ethyl] guanidine
Dozi zinazo patikana
Dozi ya kuchoma kwa sindano;
Miligramu 150/mL
Dozi ya kimiminika;
Miligramu 30/5mL
Dozi ya vidonge;
Miligramu 200
Miligramu 300
Miligramu 400
Miligramu 600
Miligramu 800
Matumizi ya dawa ya cimetidine
Dawa hii inatumika kutibu hali zifuatazo;
Vidonda vya tumbo
Kiungulia
Kucheua gesi (ugonjwa wa Gastroesofajio refluksi)
Kutibu michubuko kwenye koo la chakula iliyo sababishwa na michubuko ya tindikali (kiungulia).
Husaidia kuzuia damu kuvuja kwenye njia ya juu ya mfumo wa chakula.
Hutumiwa wakati mgonjwa akipewa dawa ya usingii kwa dharura ili kuzuia mgonjwa asipaliwe na tindikali kutoka tumboni.
Kutibu hali ya kutengenezwa kwa tindikali kupita kiasi tumboni (sindromu ya Zollinger-Ellison).
Namna dawa inavyofanya kazi mwilini
Dawa hii inazuia kutengenezwa kwa tindikali tumboni hususani mara baada ya kula chakula. Kwa kuzuia kuzalisha tindikalia inasaidia kutibu kingulia na vidonda vya tumbo na shida nyingine kutokana na tindikali tumboni.
Mwili unachofanya kwa dawa hii
Hufyonzwa kwa asilimia 60-70 kutoka kwenye mfumo wa chakula baada ya kumezwa.
Huanza kufanya kazi dakika 30, baada ya kumeza.
Ufanyaji kazi wake hufika kilele baada ya saa 1 – 3.
Huweza kufanya kazi mwilini kwa saa 4- 8.
Dawa hii huchakatwa na mwili kwenye ini ili kufanya kazi na kuondoa sumu.
Nusu Maisha ya dawa hutumika mwilini baada ya saa 2.
Taka mwili za dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo.
Maudhi madogo madogo
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Usingizi
Maumivu ya kichwa
Kuchanganyikiwa hususani kwa wazee
Kizunguzungu
Mara chache inaweza kupunguza uwezo wa kufanya tendo kwa wanaume.
Pia imeripotiwa kuwa matumizi ya muda mrefu sana yanaweza kusababisha mwanaume kuota maziwa kama wanawake. Hili ni kwa 0.1% hadi 0.2%.
Matumizi ya dawa hii kupita mshipa yanaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi, au shinikizo la damu kushuka.
Marufuku kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na cimetidine.
Muingiliano na dawa nyingine
Dawa zifuatozo hupunguza ufyonzwaji wa cimetidine;
Sodium bicarbonate
Calcium carbonate
Magnesium dihydroxide
Magnesium carbonate
Magnesium trisilicate
Aluminium hydroxide
Metoclopramide
Dawa zifuatazo huongeza uwezekano wa madhara mwilini kama zikitumiwa pamoja na cimetidine;
Anisindione
Warfarin
Heparin
Phenytoin
Quinidine
Lidocaine
Theophylline
Kutumia cimetidine pamoja na morphine kunaongeza hatari ya kushindwa kupumua.
Cimetidine hupunguza kiwango cha digoxin kwenye damu kama zikitolewa kwa pamoja.
Muingiliano na chakula
Epuka kunywa pombe unapotumia cimetidine.
Unaweza kutumia na pamoja na chakula.
Punguza matumizi ya vinywaji vyenye kafein kama vile kahawa.
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa ya cimetidine ipo katika kundi B la usalama wa dawa wakati wa ujauzito.
Matumizi kwa wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Dawa inaweza kutumika; Majaribio kwa wanyama yameonesha madhara na majaribio kwa binaadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama yameonesha madhara kidogo na majaribio kwa binadamu hayajaonesha madhara.
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Wakati wa kunyonyesha ni vyema kuepuka matumizi ya cimetidine wakati wa kunyosha na kutumia dawa salama Zaidi ili kuepuka madhara kwa mtoto anye nyonya.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-