Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
24 Aprili 2020, 06:11:58

Clozapine
Clozapine ni dawa kizazi kipya katika kundi la dawa za atipiko antisaikotiki, dawa hii hufahamika kama serotonini na dopamine inhibita kwa kuwa huzuia ufanyaji kazi wa homoni ya serotonin na dopamine kwenye mfumo wa kati wa fahamu ili kuleta madhara ambayo ndo kiini cha tiba yake. Clozapine hutumiwa katika matibabu ya ugonjwa wa skizofrenia iliyo sugu kwenye dawa tiba elekezi.
Dawa hii inapaswa kutumika lisaa limoja kabla au baada ya kula, haipaswi kutumika pamoja na chakula kwa kuwa ufyonzaji wake hupugua.
Mara baada ya kunywa dawa hii, inachukua muda wa wiki kadhaa (wiki 6 kwa mgonjwa wa skizofrenia) kabla ya dalili kuanza kupotea, unashauriwa kuendelea kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari wako katika kipindi hiko.
Ufyonzwaji wa dawa tumboni
Dawa hii mara unapoinywa hufyonzwa kwenye utumbo kwa asilimia 90 hadi 95 ya dawa. Ndani ya saa 1-2 dawa hufikia kilele chake kwenye damu.
Uchakatuaji wa dawa mwilini
Umetaboli inafanyika kwenye Ini na mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya kinyesi kwa asilimia 30 na asilimia 50 kwa njia ya mkojo.
Dawa hii hutibu
Kudhibiti halusinesheni
Kupunguza dalidali za mhemko kuhusishwa na wasiwasi
Kuthibiti mawazo yakujirudia ya kutaka kijidhuru ama kujiua
Kutibu matatizo ya usingizi
Kutibu ugonjwa wa kihisia
Maudhi madogo madogo ya dawa
Agranulosaitosisi
Kichefuchefu na kutapika
Kupata kiungulia
Kuharisha
Upele katika ngozi
Kizunguzungu
Kuongezeka hamu ya chakula
Kuvimbiwa
Maumivu ya tumbo
Ongezeko la uzito wa mwili
Kutokwa na jasho jingi
Kuweweseka
Maumivu ya kichwa
Kuanguka
Kusinzia
Udhaifu wa mwili
Haipagkaisemia
Dayabetiki ketoasidosisi
Angalizo
Tumia dawa hii kwa Umakini kwa watu
Wenye matatizo ya Ini
Wenye shinikizo la damu, matatizo sugu ya moyo
Wenye matatizo ya Kifafa
Wenye matatizo ya Figo
Wenye aleji na dawa hii na pamoja na aleji nyingine
Wenye matatizo ya kukosa fahamu
Wenye magonjwa ya damu mfano leukemia
Wenye kisukari
Usitumie dawa hii pamoja na
Usitumie dawa hii pamoja na dawa za kutibu shinikizo la damu la juu
Usitimie dawa hii pamoja na dawa jamii ya antidepressants mfano fluvoxamine
Usitumie dawa hii pamoja na baadhi ya antibiotiki mfano ciproflaxin
Usitumie dawa hii pamoja dawa za kifafa mfano carbamazepine
Usitumie kama unamzio na dawa hii
Kwa Wajawazito
Itumiwe endapo kuna umuhimu katika ujauzito
Kwa Wanaonyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyeshwa.
Ukisahau dose Nini kifanyike
Kama umesahau kunywa dose yako, kunywa mara tu unapokumbuka, endapo muda wa dozi nyingine umefika, ruka hiyo dozi uliyosaau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:46:38
Rejea za mada hii:-