Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
8 Septemba 2021 18:09:22
Dawa Cefotaxime
Cefotaxime ni moja ya antibiotiki ya kizazi cha tatu cha cephalosporin inayotumika kutibu maambukizi mbalimbali ya bakteria mwili. Inatumika kwa bakteria wa gram hasi na gram chanya na ipo katika kundi la tatu la dawa
Majina mengine ya Cefotaxime
Cefotaxime kwa jina linguine hufahamika kama Claforan.
Dawa zilizo kundi moja na Cefotaxime
Dawa zilizo kundi moja na cefotaxime ni ;
Ceftriaxone
Cefixime
Ceftibuten
Ceftazidime
Fomu ya dawa
Dawa hii ipo katika fomu ya Unga kwa ajiri ya Sindano
Uzito wa dawa
Unga kwa ajiri ya sindano upo katika uzito wa miligramu 500 kwa chupa moja
Cefotaxime hutibu nini?
Hutibu maambukizi katika mfumo wa mkojo
Hutibu Nimonia
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye via vya uzazi (PID)
Hutibu maambukizi kwenye uti wa mgongo
Hutibu maambukizi kwenye mfumo wa hewa
Hutumika kama kinga kabla wakati na baada ya upasuaji
Hutumika kutibu kaswende
Hutumika kutibu sepsisi na septisemia
Hutibu maambukizi kwenye ngozi
Hutibu maambukizi kwenye mifupa na viungio vya mwili
Hutibu Peritonaitis
Hutibu maambukizi ya bakteria kwneye ubongo
Hutibu homa ya lyme
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye ubongo
Namna Cefotaxime inavyoweza kufanya kazi
Cefotaxime hufanya kazi ya kuua na kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa ukuta wa cell ya bakteria husika kupitia uwezo wake mkubwa wa kujishikiza kwenye protini muhimu ambayo penicillin pia hujishikiza.
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri inavyotolewa ndani ya misuli na ndani ya mishipa.
Vimelea wanaodhuriwa na Cefotaxime
Enterococcus spp
Staphylococcus spp
Streptococcus spp
Acinetobacter spp
Citrobacter spp
Enterobacter spp
Escherichia coli
Haemophilus spp
Klebsiella spp.
Neisseria spp
Proteus spp
Mwingiliano wa Cefotaxime na chakula
Hakuna chakula rasmi unachotakiwa acha kwenye mlo wako unapotumia dawa hii.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cefotaxime
Wagonjwa wenye mzuio wa hii na dawa nyingine jamii ya Cephalosporin.
Wagonjwa wenye mzio wa Penicillin.
Dawa zenye muingiliano na Cefotaxime
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Cefotaxime;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya kipindupindu
Chanjo hai ya Typhoid
Dawa zinazoweza kutumika na Cefotaxime chini ya uangalizi;
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Dienogest/estradiol valerate
Ethinylestradiol
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Probenecid
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Ticarcillin
Warfarin
Dawa zenye muingiliano mdogo na cefotaxime;
Aminohippurate sodium
Chloramphenicol
Choline magnesium trisalicylate
Rose hips
Sulfasalazine
Willow bark
Maudhi madogo ya Cefotaxime;
Kichefuchefu
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kuzimia
Kuvimba uso,macho,ulimi,mikono,miguu na tezi
Homa
Maumivu ya kifua
Kushindwa kupumua
Kutapika
Kuwasha mwilini na kupata vipele
Kushindwa kumeza
Kizunguzungu
Kupata kiu ya mara kwa mara
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Maumivu wakati wa kukojoa na kooni
Damu kwenye mkojo, Fizi na choo
Kupungua uzito
Matumizi ya cefotaxime kwa mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Cefotaxime kwa mama mjamzito
Mpaka sasa hakuna tafiti inayoonyesha madhara ya cefotaxime kwa mama mjamzito. Ingawa tafiti nyingi zinaonesha kuwa wanyama wajawazito walipewa dawa hii, watoto wao hawakuonyesha madhara yoyote.
Matumizi ya Cefotaxime kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha hivyo chagua kuacha kutumia dawa au kunyonyesha mtoto n ahata hivyo umuhimu wa dawa kwa mama unapaswa kuzingatiwa.
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu kupata dawa hii kwa wakati sahihi. Ukikosea dozi muulize daktari au mfamasia ratiba mpya ya dozi. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja ili kufidia dozi uliyoikosa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-