Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
7 Septemba 2021, 13:43:15
Dawa Ceftriaxone
Ceftriaxone ni moja ya antibiotiki ya kizazi cha tatu cha kundi la Cephalosporins yenye wigo mpana wa kuua vimelea aina ya Aerobic na Anaerobic, gramu hasi na gramu chanya . Majina mengine ya dawa hii ni Rocephin
Fomu na uzito wa ceftriaxone
Ceftriaxone hupatikana katika fomu ya unga ambao huchanganywa na maji maalumu kisha kuchomwa kwenye mshipa wa damu au misuli
Uga huwa na uzito wa gramu 1 kwa kila chupa
Dawa zilizo kundi moja na Ceftriaxone
Dawa zilizo kundi moja na cefriaxone ni ;
Ceftriaxone
Cefdinir
Cefixime
Cefpodoxime
Cefditoren
Ceftibuten
Cefdinir
Ceftazidime
Ceftazidime
Cefotaxime
Ceftazidime
Cefoperazone
Ceftizoxime
Upekee wa ceftriaxone na dawa zilizo kundi moja
Ceftriaxone huwa na nusu maisha marefu kuliko dawa zingine kwenye kundi lake na hivyo kufanya itumike mara moja kwa siku na kuwa dawa nzuri kutumika kwa wagonjwa wa ndani nan je.
Dawa hii pia huwa na uwezo wa kupita katika ukuta wa uongo na kuingia ndani ya ubongo hivyo kuweza kutumika kwa matibabu ya homa ya uti wa mgongo.
Mbali na sifa hizo, dawa kwenye kundi la tatu la cephalosporin huwa na maudhi kidogo
Ceftriaxone hutibu nini?
Hutibu maambukizi katika mfumo wa mkojo
Hutibu maambukizi kwenye koo na masikio
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye via vya uzazi
Hutibu maambukizi ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo kutokana na bakteria
Hutibu maambukizi kwenye mfumo wa hewa
Hutumika kama kinga kabla na baada ya upasuaji
Hutumika kutibu kaswende na kisonono
Hutumika kutibu sepsisi na septikemia
Hutibu maambukizi kwenye ngozi
Namna Ceftriaxone inavyoweza kufanya kazi na ufyonzwaji wake
Namna inavyofanya kazi
Ceftriaxone hufanya kazi ya kuua bakteria kwa kuzuia ufanyaji kazi wa vimeng’enya muhimu vya bakteria vinavyohusika kutengeneza ukuta wa bakteria.
Ufyonzwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri inavyotolewa ndani ya misuli na ndani ya mishipa.
Vimelea wanaodhuriwa na Ciprofloxacin
Proteus mirabilis
Escherichia coli
Haemophilus Influenza
Klebsiella pneumonia
Pseudomonas aeruginosa
Neisseria Meningitis
Streptococcus spp
Staphylococcus spp
Clostridium spp
Enterobacter spp
Dawa zenye muingiliano na Ceftriaxone
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ceftriaxone;
Chanjo ya BCG
Heparin
Warfarin
Argatroban
Bivalirudin
Tinzaparin
Calcium gluconate
Dalteparin
Calcium acetate
Calcium Carbonate
Calcium Chloride
Calcium Citrate
Calcium Gluconate
Dawa zinazoweza kutumika na Ceftriaxone chini ya uangalizi;
Argatroban
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Chanjo hai ya BCG
Bivalirudin
Chloramphenicol
CHanjo ya kipindupindu
Dalteparin
Demeclocycline
Doxycycline
Enoxaparin
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Fondaparinux
Heparin
Lepirudin
Minocycline
Tetracycline
Tinzaparin
Chanjo hai ya typhoid
Warfarin
Dawa zenye muingiliano mdogo na cefriaxone;
Furosemide
Rose hips
Choline magnesium trisalicylate
Gome la Willow
Mwingiliano wa Ceftriaxone na chakula
Dawa hii unaweza kuitumia ukiwa umekula ama bila kula. Tafiti zinaonyesha kuwa ceftriaxone haina mwingiliano wowote na chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ceftriaxone
Wagonjwa wenye mzio wa hii dawa na zingine jamii ya Cephalosporin.
Wagonjwa wenye mzio wa Penicillin
Utoaji taka wa Ceftriaxone mwilini
Kiwango kikubwa cha ceftriaxone tulolewa kwa njia ya mkojo na kiwango kidogo kwa njia ya haja kubwa.
Matumizi ya Ceftriaxone kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Mpaka sasa hakuna tafiti inayoonyesha madhara ya ceftriaxone kwa mama mjamzito.
Matumizi ya Ceftriaxone kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha lakini haitegemei kuleta madhara kwa mtoto anayenyonya. Hivyo inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Ceftriaxone
Kichefuchefu
Kuharisha
Maumivu ya kichwa
Kuzimia
Kuvimba uso,macho,ulimi,mikono,miguu
Kichefuchefu
Maumivu ya kifua
Kushindwa kupumua
Kutapika
Kuwasha mwilini
Husababisha manjano
Kizunguzungu
Maumivu ya tumbo
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu kupata dawa hii kwa wakati sahihi.Ukikosea dozi muulize daktari au mfamasia ratiba mpya ya dozi, Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja ili kufidia dozi.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-