Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Septemba 2021 18:22:49
Dawa Flibanserin
Flibanserin ni dawa jamii ya Serotonin 5-HT-risepta agonist, inayotutumika kwa wanawake ambao hawajaingia komahedhi kutibu madhaifu yenye ya kupungua kwa hisia za kingono kwa ujumla yanayoambatana na masumbufu binafsi au ya mahusiano. Matatizo ya kingono yanayotibiwa na dawa hii si yale yanayosababishwa na matatizo ya kiakili, magonjwa au matumizi ya dawa zinazopunguza ufanisi wa kingono.
Jina jingine la Flibanserin
Flibanserin hufahamika kwa jina jingine la; Addyi
Fomu na uzito wa Flibanserin
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa Milligramu 100
Flibanserin hutibu nini?
Hutibu madhaifu ya hamu kidogo ya ngono yaliyodumu angalau kwa muda wa miezi sita na kuendelea na yanayoambatana na masumbufu binafsi au ya mahusiano
Baadhi ya dalili za madhaifu ya hamu kidogo ya ngono ni;
Kupungua kwa mawazo au muwasho wa kingono wakati wa ngono Kupungua au kupotea kwa msisimuko wakati wa ngono Kukosa uwezo wa kuendelea kuwaza ngono au kusisimuka wakati wa ngono Kukosa hamu ya kufanya ngono
Matumizi ya flibanserin nje ya malengo
Addyi huweza kutumika kuongeza hisia za ngono na kufika kileleni kirahisi kwa mtu asiye na tatizo la kingono. Matumizi haya hayajaruhusiwa na FDA.
Namna Flibanserin inavyoweza kufanya kazi
Flibanserin ni serotonin-1A (5HT-1A) risepta agonist na 5HT-2A risepta agonist, pia huwa na madhara kiasi upingamizi kwenye risepta za 5-HT2B, 5-HT2C na dopamine D4 Haifahamiki vema namna gani Flibanserin inavyofanya kazi, inafikiriwa kurejesha uwezo wa sehemu ya ubongo wa mbele kudhibiti mfumo wa zawadi/motisha na hivyo kusababisha ongezeko la hamu ya ngono. Hii huonekana kwa kusababisha ongezeko la homon dopamine na norepinephrine wakati kupungua kwa homon serotonin katika sehemu ya mbele ya ubongo.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia flibanserin
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au zingine jamii yake.
Tahadhari kwa watumiaji wa flibanserin
Haipaswi kutumika pamoja na kilevi chochote kwa sababu pombe huongeza kushuka kwa shinikizo la damu na kupoteza fahamu kwa muda kama ikitumiwa pamoja na flibanserin
Unaweza kusubiria angalau masaa 2 kupita baada ya kunywa pombe ndipo utumie dawa
Kama umekunywa bia zaidi ya mbili kwa siku, unapaswa kuruka dozi ya dawa ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. Hata hivyo ULYCLINIC inakushauri usitumie kilevi chochote wakati unatumia dawa hii.
Haipaswi kutumika kwa watu wenye matatizo ya ini
Utoaji taka wa flibanserin
Asilimia 51 hutolewa kwa njia ya kinyesi na 44 kwa njia ya mkojo
Mwingiliano wa flibanserin na dawa zingine
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutoruhusiwa kutumika pamoja na flibanserin;
Abametapir
Amiodarone
Aprepitant
Atazanavir
Bicalutamide
Ceritinib
Ciprofloxacin
Clarithromycin
Clozapine
Cobicistat
Conivaptan
Crizotinib
Cyclosporine
Darunavir
Desipramine
Diltiazem
Doxycycline
Dronedarone
Elvitegravir/cobicistat/emtricitabine/tenofovir df
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Ethanol
Fluconazole
Fosamprenavir
Grapefruit
Haloperidol
Idelalisib
Iloperidone
Imatinib
Indinavir
Isoniazid
Itraconazole
Ketoconazole
Lapatinib
Lidocaine
Lopinavir
Metronidazole
Nefazodone
Nelfinavir
Netupitant/palonosetron
Nicardipine
Posaconazole
Quinidine
Ritonavir
Saquinavir
Schisandra
Sertraline
Tetracycline
Ticagrelor
Tipranavir
Verapamil
Voriconazole
Zileuton
Dawa hizi zina mwingiliano mkali hivyo tumia dawa nyingine badala ya
Amobarbital
Apalutamide
Colchicine
Eslicarbazepine acetate
Fexinidazole
Ivosidenib
Lonafarnib
Lorlatinib
Metoclopramide a kuweka puani
Ozanimod
Ribociclib
Rimegepant
Secobarbital
Tucatinib
Venetoclax
Voxelotor
Primaquine ikitumika na dawa hizi mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu
Acetaminophen
Acetaminophen IV
Acetaminophen a kuweka kwenye puru
Acetazolamide
Alprazolam
Amlodipine
Amobarbital
Anastrozole
Aripiprazole
Armodafinil
Asenapine
Atorvastatin
Azelastine
Benzhydrocodone/acetaminophen
Berotralstat
Betamethasone
Betrixaban
Bortezomib
Bosentan
Brexanolone
Bromocriptine
Brompheniramine
Buprenorphine
Buprenorphine buccal
Buprenorphine subdermal- kipandikizi
Buprenorphine transdermal
Butabarbital
Butalbital
Butorphanol
Cannabidiol
Carbamazepine
Carbinoxamine
Cariprazine
Cenobamate
Chloral hydrate
Chloramphenicol
Chlordiazepoxide
Chlorpheniramine
Chlorzoxazone
Cimetidine
Clemastine
Clonazepam
Clonidine
Clorazepate
Clozapine
Cocaine
Codeine
Crofelemer
Cyclophosphamide
Cyclosporine
Cyproheptadine
Dabrafenib
Danazol
Darifenacin
Dasatinib
Desvenlafaxine
Dexamethasone
Dexchlorpheniramine
Dexlansoprazole
Dexmedetomidine
Diazepam
Diclofenac
Digoxin
Dihydroergotamine
Dimenhydrinate
Diphenhydramine
Disulfiram
Docetaxel
Doxorubicin
Doxorubicin liposomal
Doxylamine
Drospirenone
Duvelisib
Efavirenz
Elagolix
Enzalutamide
Ergotamine
Esketamine a kuweka puani
Estazolam
Eszopiclone
Ethinylestradiol
Etoposide
Etravirine
Fedratinib
Felodipine
Fenfluramine
Fentanyl
Fentanyl a kuweka puani
Fentanyl transdermal
Fentanyl transmucosal
Fexinidazole
Fluconazole
Fluoxetine
Fluphenazine
Flurazepam
Fluvastatin
Fluvoxamine
Fosphenytoin
Gemfibrozil
Ginkgo biloba
Glecaprevir/pibrentasvir
Glyburide
Haloperidol
Hydralazine
Hydrocodone
Hydromorphone
Hydroxyzine
Ifosfamide
Iloperidone
Irbesartan
Isoniazid
Isradipine
Istradefylline
Lansoprazole
Lasmiditan
Lemborexant
Lenvatinib
Levorphanol
Lomustine
Lorazepam
Losartan
Lovastatin
Loxapine
Loxapine inhaled
Lumacaftor/ivacaftor
Lurasidone
Mefloquine
Meperidine
Mestranol
Methadone
Methimazole
Methoxsalen
Methylprednisolone
Micafungin
Midazolam
Midazolam a kuweka puani
Mifepristone
Mirtazapine
Mitotane
Mitoxantrone
Modafinil
Molindone
Morphine
Nafcillin
Nalbuphine
Naldemedine
Nevirapine
Nifedipine
Nisoldipine
Nizatidine
Olanzapine
Oliceridine
Omeprazole
Orphenadrine
Oxazepam
Oxcarbazepine
Oxybutynin
Oxybutynin transdermal
Oxycodone
Oxymorphone
Palbociclib
Paliperidone
Paroxetine
Pazopanib
Pentamidine
Pentazocine
Pentobarbital
Perphenazine
Phenobarbital
Phenytoin
Pilocarpine
Pimavanserin
Pimozide
Pravastatin
Prednisolone
Primaquine
Primidone
Progesterone micronized
Promethazine
Propofol
Quazepam
Quetiapine
Quinine
Rabeprazole
Ramelteon
Ranolazine
Remifentanil
Rifabutin
Rifampin
Rifapentine
Risperidone
Rucaparib
Secobarbital
Selegiline
Selegiline transdermal
Sirolimus
St john's wort
Stiripentol
Sufentanil
Sufentanil sl
Sulconazole
Suvorexant
Tacrolimus
Talazoparib
Tamoxifen
Tapentadol
Tasimelteon
Tazemetostat
Tecovirimat
Temazepam
Temsirolimus
Teniposide
Testosterone
Testosterone ya kupaka
Thiothixene
Ticlopidine
Tramadol
Tranylcypromine
Trazodone
Triazolam
Triclabendazole
Trifluoperazine
Triprolidine
Valproic acid
Vinblastine
Vincristine
Vincristine liposomal
Vinorelbine
Zafirlukast
Zaleplon
Ziprasidone
Zolpidem
Matumizi ya flibanserin kwa mama mjamzito
Hakuna tafiti kwa binadamu zinazoonyesha madhara yake kwa kijusi tumboni, hata hivyo tafiti za wanyama zinaonyesha kuwa kusababisha kuzaliwa na uzito kidogo na wakiwa kwenye kaputi.
Matumizi ya Primaquine kwa mama anayenyonyesha
Haijulikana kama inaingia kwenye maziwa ya mama. Hata hivyo dawa huingia kwenye maziwa ya wanyama licha ya kutofahamika kama flibanserin inasababisha madhara kwa kichanga anayenyonya au kudhuru uzalishaji wa maziwa.
Maudhi na madhara ya flibanserin
Maudhi ya kawaida ya flibanserin ni pamoja na;
Haja kubwa ngumu
Kukauka kwa midomo
Kuwa na shauku
Kubadilika kwa hedhi
Harara kwenye ngozi
Kukosa usingizi
Madhara ya flibanserin
Flibanserin inaweza kusababisha maudhi makubwa kwa baadhi ya watumiaji, onana na daktari haraka kama utapata dalili zifuatazo;
Kuvimba
Kupumua kwa shida
Kuvimba uso, midomo, ulimi au kinywa
Uono hafifu
Kuchanganyikiwa
Kizunguzungu
Kuzimia
Hisia za kichwa chepewi
Usingizi
Hisia za kulewa
Kutokwa na jasho
Kuchoka kusiko kawaida
Hisia za vitu vinazunguka
Tumbo kujaa gesi
Homa
Kichefuchefu
Dalili kali ya kubana kwa misuli
Maumivu ya tumbo la chini
Kutapika
Je endapo umesahau dozi yako ufanyaje ?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapo kumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana ambapo utatakiwa kuruka dozi uliyosahau kisha kuendelea na dozi inayofuata katika muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-