Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020 08:59:23
Dawa ya Anidulafungin
Anidulafungin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya echinocandins. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la eraxis
Fomu na uzito wa Anidulafungin
Anidulafungin hupatikana katika fomu ya unga unaochangaywa na maji kabla ya kuchoma mwilini kwa njia ya sindano. Chupa moja ya unga huwa na dawa yenye uzito wa Milligram 50
Namna Anidulafungin inavyofanya kazi
Dawa ya anidulafungin ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi ya kuzuia utengenezwaji wa kiungo kinachoitwa glucan ambacho ni moja ya kiungo muhimu katika ukuta wa seli ya fangasi . Dawa hufanikisha jukumu hilo kwa kuzuia kimeng’enya kinachoitwa Glucan synthase kufanya kazi hivyo kuzuia ukuaji wa seli ya fangasi
Dawa zilizo kundi moja na Anidulafungin
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo: • Micafungin • Capsofungin
Kazi ya Anidulafungi
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi wa kooni, waliosambaa kwenye mrija wa esofagasi au kwenye damu
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Anidulafungin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo: • Deflazacort • Dichlorphenamide • Sodium sulfate • Potassium sulfate
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Anidulafungin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Tahadhari kwa watumiaji wa Anidulafungin
Dawa hii huweza kupelekea matatizo kwenye ini Huweza kusababisha kubana kwa mirija ya kupitisha hewa katika mfumo wa upumuaji
Utofauti wa Anidulafungin kwenye kundi la Echinocandins
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya kinyesi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko kwa njia ya mkojo. Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni nusu saa hadi saa 1 tangu itumike mwilini
Matumizi ya Anidulafungin wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi ya Anidulafungin wakati wa kunyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya Anidulafungin kwa watumiaji
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : • Kuharisha • Haipokalemia • Kichefuchefu • Ngozi kuwasha
Ukisahau dozi ya Anidulafungin
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa a mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-