Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
7 Julai 2020 16:42:18
Dawa ya Clotrimazole
Clotrimazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi.
Majina ya kibiashara
Clotrimazolehufahamika pia kama
Canesten
Labesten n.k
Fomu na uzito
Dawa ya Clotrimazole hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa miligramu 10 au fomu ya krimu wenye ujazo mbalimbali na mfumo wa vidongevya kuweka ukeni
Ufanyaji kazi wa Clotrimazole
Dawa jamii ya Antifangasi ikiwemo Clotrimazole hufanya kazi zifuatvyo ili kutibu fangasi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuharibu ukuta wa seli wa fangasi, kuharibika huku hufanya fangasi wafe. Huharibu kwa kuzuia utengenezaji wa egosteroli, hiki ni kiungo muhimu sana kwenye ukuta wa seli wa fangasi kwa kuwa hufanya kazi kama homoni ili kusaidia seli ya fangasi itengeneze ukuta wake.
Dawa kundi moja na Clotrimazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Ciclopiro
Econazole
Fluconazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Ketoconazole
Miconazole
Naftifine hydrochloride
Nystatin
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terbinifine
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Clotrimazole hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi kwenye mfumo wa umeng'enyaji wa chakula uliyosababisha na Kandidiasi pamoja na fangasi wa ukeni
Clotrimazole na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Elagolix
Everolinus
Lomitapide
Axitinib
Bosutinib
Eliglustat
Warfarin
Wagonjwa wasiopaswa kutumia clotrimazole
Clotrimazole haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Tahadhali ya clotrimazole
Clotrimazole inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye shida ya magonjwa ya Ini.
Upekee wa clotrimazole
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni;
Dawa hii huwa na uwanja mpana wa kutibu fangasi aina tofauti, hivyo huchukuliwa kama dawa bora, hata hivyo mbali na uwezo wake wa kutibu fangasi, imekuwa ikutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa seli mundu, malaria na baadhi ya saratani
Huwa na maudhi machache na umeng’enyaji wake hueleweka ndo maana inakubalika sana maeneo mengi duniani kutumia kutibu fangasi wa ukeni na miguuni
Clotrimazole na ujauzito
Itumike kwa uangalifu kipindi cha ujauzito, dawa ya kupaka na vidonge vya kuweka kwenye uke ni salama zaidi kuliko vidonge kwa kunywa.
Clotrimazole kipindi cha kunyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila haishauriwi itumike kwa wamama wajawazito
Maudhi madogo ya clotrimazole
Kichefuchefu
Kutapika
Kuhisi kuungua
Kuwashwa mwili
Je, kama umesahau dozi ya clotrimazole?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Clotrimazole, tumia mara pale utakapokumbuka kisha endelea kwa muda kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-