Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020, 06:20:22
Dawa ya Doxycycline
Doxycycline ni antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kutibu magonjwa yanayotokana na maambukizi ya bakteria.
Majina mengine
Doxycycline huwa maarufu kwa majina ya Vibramycin na monodox.
Muda wa kuanza kazi
Doxycycline hufanya kazi pale inaponyewa Saa 1 au masaa 2 baada ya kula
Fomu ya dawa
Doxycycline hupatikana katika mfumo wa tembe wenye uzito wa;
50 mg
75 mg
100 mg
150 mg
Ufanyaji kazi wa doxycycline
Doxycycline hufanya kazi kwa kushikamana na Ribosome ya bakteria inayohusika kuzalisha protini muhimu zinazojenga mwili wa bakteria. Bila kuwa na hizi protini bakteria hukosa uwezo wa kufanya kazi zake kuleta madhara kwenye mwili. Hivyo Doxycycline hufanya kazi ya kusimamisha uzalishaji wa bakteria badala ya kuua bakteria.
Dawa zilizo kwenye kundi moja na Doxycycline
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Doxycycline ( yaani kundi la tetracyclline) ni;
Choltetracycline
Oxytetracycline
Tetracycline
Minocycline
Demecycline
Methacyxline
Rolitetracyxline
Doxycycline hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono
Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa hewa yanayosababishwa na bakteria aina ya mycoplasma pneumoniae
Matumizi ya Doxycycline nje ya kazi yake
Doxycyline hutumika pamoja na dawa Ivermectin na madini zinck katika matibabu ya Ugonjwa wa COVID-19. Hii ni kutokana na tafiti zilizofanyika bara la Amerika na kuonyesha kuwa dawa hii ikitumika pamoja na dawa zilizotajwa, zinauwezo wa kupunguza kwa kasi dalili za COVID-19 pamoja na kuharakisha kupona ugonjwa kwa wagonjwa wenye dalili kali na dalili za kawaida Hata hivyo tafiti zinaonyesha kuwa, hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu dawa Ivermectin kutumika kwenye matibabu ya COVID-19 na zinaita kufanyika tafiti nyingi kufanyika zaidi ili kutoa majibu mazuri yenye uhakika.
Upekee wa Doxycycline
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 15 hadi 20 tangu itumike mwilini
Dawa hii hutolewa kwa njia ya kinyesi zaidi ukilinganisha na mkojo
Mwingiliano na dawa zingine
Doxycycline haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acitretin
Flibanserin
Lomitapide
Tretinoin
flibanserin
lomitapide
tretinoin
Aluminum hydroxide
Aminolevulinic acid
Amoxicillin
Ampicillin
Apalutamide
Atracurium
Avapritinib
Axitinib
Bismuth subsalicylate
Bosutinib
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Carbonyl iron
Cisatracurium
Cobimetinib
Dicloxacillin
Eliglustat
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Doxycycline
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline
Wagonjwa wa ini
Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni
Tahadhari ya Doxycycline
Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo
Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8
Doxycycline na ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapo hairuhusiwi kutumika. Soma zaidi kwenye usalama wa dawa wakati wa ujauzito kwa maelezo zaidi.
Doxycycline kipindi cha kunyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya doxycycline
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kutapika
Kuvimba mdomo
Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo
Je endapo utasahau dozi yako ya doxycycline ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako ya doxycycline, tumia mara pale utakapokumbuka. Ikiwa muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiri ufike ili utumie dozi hiyo kama ulivyopangiwa na daktari.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-