Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
7 Julai 2020 19:30:46
Dawa ya Fluconazole
Fluconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. hutibu fangasi wa juu ya ngozi na waliosambaa kwenye damu.
Majina mengine ya fluconazole;
• Afungil • Apo-fluconazol • Azoflune • Beagyne • Bioxel • Biozole • Candizol • Canesten oral • Conasol • Diflazole • Diflazon • Diflucan • Difluzol • Dom-fluconazole • Elazor • Felsol • Figalol • Fluc • Flucan • Flucandid • Flucanol • Flucazol • Flucobeta • Flucol • Flucolich • Flucoltrix • Fluconabene • Fluconal • Fluconazol • Fluconazole omega • Fluconeo • Flucosept • Flucoxan • Flucozal • Flucoz • Flucozen • Flucozole • Fluctin • Fludizol • Fludocel • Flukazol • Flukeno • Flunazol • Flunazul • Flunco • Fluotec • Flusan • Flusenil • Flutec • Fluzor • Funa • Fungal • Fungata • Fungustatin • Fungusteril • Gen-fluconazole • Glyfucan • Gynosant • Hadlinol • Helmicin • Ibarin • Kyrin • Lavisa • Lertus • Loitin • Micofin • Monipax • Mycomax • Mycosyst • Neofomiral • Nesporac • Novo-fluconazole • Nu-flucon • Oxifungol • Pantec • Plusgin • Pms-fluconazole • Pronazol • Reforce • Riconazol • Solacap • Stabilanol • Stalene • Supremase • Tavor • Teczol • Tierlite • Triazol • Trican • Triflucan • Unizol • Waynazol • Zelix • Zidonil • Zolanix • Zoldicam • Zolmic • Zolstatin • Zoltec • Zoltren • Zonal
Rangi na fomu ya dawa ya Fluconazole
Rangi yake huwa mara inatofautiana na mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza. Fluconazole hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa; • 50mg • 100mg • 150mg na • 200mg Fluconazole hupatikana katika mfumo wa kimiminika kwa ajili ya kunywa chenye ujazo wa ; • Miligramu 10 kwa mililita (10mg/ml) • Miligramu 40 kwa mililita (40mg/ml) Fluconazole hupatikana katika mfumo wa kimiminika kwa ajili ya sindano chenye ujazo 2mg/ml Fluconazaole pia hupatikana kwenye fomu ya krimu kwa ajili ya kupaka.
Namna Fluconazole inavyofanya kazi
Dawa ya Fluconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi, Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng’enya cha saitokromu P-450 ambacho ni muhimu inayohusika kuzalisha homoni ya ergosteroli kutoka kwenye kiungo lanosteroli. Homoni hii huwa muhimu katika ukuta wa seli za fangasi, kukosekana kwa homoni hii katika kuta hufanya kuta hizo kuwa dhaifu na fangasi hufa.
Dawa zilizo kundi moja na Fluconazole
• Amphotericin B • Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Econazole • Flucytosine • Griseofulvin • Itraconazole • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole
Fluconazole hutibu nini?
Fluconazole hutumika kwenye matibabu ya; • Maambukizi ya fangasi ukeni • Maambukizi ya fangasi kwenye damu • Maambukizi ya fangasi kwenye kinywa na umio • Homa ya uti wa mgongo kutokana na fangasi (Cryptococcal meningitis) • Maambukizi ya fangasi kwenye peritoniamu
Vimelea wanaodhuriwa na fluconazole
• Candida albicans • Candida glabrata( kwa wastani) • Candida parapsilosis • Candida tropicalis • Cryptococcus neoformans
Nusu maisha ya dawa na njia ya utolewaji mwilini
Nusu maisha ya dawa fluconazole ni wastani wa 30 (kati ya masaa 20 hadi 50), asilimia 80 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo bila kufanyiwa umetaboli, wakati asilimia 11 hutolewa kama mazao mengine baada ya kufanyiw aumetaboli na ini.
Dawa marufuku kutumia pamoja na Fluconazole
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo; • Disopyramide • Erythromycin base • Erythromycin ethylsuccinate • Erythromycin lactobionate • Erythromycin stearate • Flibanserin • Ibutilide • Indapamide • Lomitapide • Pentamidine • Pimozide • Procainamide • Quinidine • Ribociclib
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Fluconazole
• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa zingine za Antifangasi • Wagonjwa wenye Magonjwa ya figo
Utofauti wa pekee wa Fluconazole na dawa zingine kwenye kundi moja
• Dawa hii hutolewa mwili kwa njia ya Ini kwa asilimia kubwa kwa njia ya mkojo. • Dawa huwa na maudhi kidogo na huweza kutibu fangasi wa ukeni kwa dozi moja tu. • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 30 tangia utumie dawa kunywa kwenye mwili.
Matumizi Fluconazole kwa mama mjamzito
Hakuna taarifa za kutosha zinazohusu matumizi ya fluconazole kwa mjamzito. Baadhi ya taarifa zinaonyesha kuwepo na uwezekano wa kupata madhaifu ya kiuumbaji kwa kichanga tumboni kama itatumika katika dozi kubwa. Hata hivyo unashauriwa kutumia dawa zingine zilizo salama zaidi au dawa ya kupaka ambayo inaingia kwenye damu kwa kiasi kidogo kama faida ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza
Matumizi Fluconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu Zinaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto hivyo inashauriwa itumike kwa wamama wanaonyonyesha kwa uangalifu mkubwa.
Maudhi ya Fluconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : • Kichefuchefu • Kutapika • Maumivu ya tumbo na kichwa • Kizunguzungu • Kuharisha • Kukosa hamu ya tendo la ndoa • Mwili kuwa manjano • Kuogopa mwanga • Kuwashwa mwili
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau tumia dozi yako, tumia mara utakapokumbuka. Kama muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata katika muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-