Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Agosti 2020 17:36:05
Dawa ya Griseofulvin
Griseofulvin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Gris-peg.
Fomu ya na uzito wa Griseofulvin
Griseofulvin hupatikana katika fomu ya idonge chenye uzito mbalimbali kama vile, •125mg •150mg na •200mg Griseofulvin pia hupatikana kwenye fomu ya kimiminika cha maji chenye ujazo wa •Miligramu 125 kwa 5 mililita (125mg/5ml)
Namna Griseofulvin inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
• Dawa jamii ya Antifangasi ikiwa pamoja na Griseofulvin hufanya kazi zifuatvyo ili kutibu fangasi kwenye ngozi, mwilini, nyewle/ndevu au kucha. • Dawa hii ya Griseofulvin na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia kuzalishwa na kuongezeka kwa seli ya fangasi • Griseofulvin pia huweka keratini kwenye seli ya ngozi na kufanya iwe na uimara na kuzuia fangasi wasiingie kwenye ngozi na tishu nyingine za mwili.
Mfano wa dawa kundi la antifangasi kama Griseofulvin
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
• Amphotericin B • Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Fluconazole • Flucytosine • Itraconazole • Ketoconazole • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole
Dawa zisizopaswa kutumika kwa pamoja na Griseofulvin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo: • Aminolevulinic Acid • Dihydroergotamine • Dihydroergotamine Intranasal • Dronedarone • Ergotamine • Erythromycin Base • Erythromycin Ethylsuccinate • Erythromycin Lactobionate • Erythromycin Stearate • Ethinylestradiol • Everolimus • Lovastatin • Methyl Aminolevulinate • Ranolazine • Silodosin • Simvastatin • Sirolimus • Tolvaptan • Tucatinib • Ulipristal
Kazi ya dawa Griseofulvin
Dawa hii siyo imara dhidi ya maradhi ya bacteria. Mamlaka ya dawa na chakula iliidhinisha dawa hii mwaka ianz ekutumika kwa maradhi ya fagasi mwaka 1959 • Griseofulvin ni dawa ni nzuri dhidi ya Microsporiamu, epidermofaitoin na trichofaitoin. • Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi waliyo kwenye ngozi na waliyosambaa sehemu mbalimbali za mwili.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Griseofulvin
• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Utofauti wa Griseofulvin na dawa zingine za kutibu fangasi
Dawa hii nusu ya maisha yake mwilni ni masaa tisa mpaka masaa 21
Matumizi Griseofulvin kipinid cha ujauzito
• Dawa hii ipo kwenye kundi X la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito • Dawa hii haishauriwa kutumika wakati wa kipindi cha ujauzito.
Matumizi Griseofulvin kipinid cha kunyonyesha
Takwimu hazionyeshi kuwa kuna huwezekano wa hii dawa kuingia au hapana kwenye maziwa ya Mama hivyo inashauriwa isitumike kwa wamama wanaonyonyesha kwasababu ina madhara kwa mtoto
Maudhi ya Griseofulvin kwa watumiaji
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : •Kichefuchefu •Kutapika •Maumivu ya tumbo na kichwa •Kizunguzungu •Kupata Homa •Kuharisha •Kukosa hamu ya tendo la ndoa •Mwili kuwa manjano •Kuogopa mwanga •Kuwashwa mwili
Je endapo utasahau kutumia dozi yako ya Griseofulvin ufanyaje ?
Endapo umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-