top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Julai 2020 08:31:46

Dawa ya Itraconazole

Dawa ya Itraconazole

Itraconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa Triazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Sporanox. Dawa hii huwa na rangi nyeupe japo huwa inatofautiana na mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza.


Majina mengine ya itraconazole


• Sporanox • Tolsura • Onmel


Fomu na uzito wa itraconazole


Dawa ya Itraconazole hupatikana kama kidonge na tembe Mfumo wa kidonge huwa na uzito wa miligramu,

• 200mg Mfumo wa tembe chenye uzito wa miligramu, • 65mg • 100mg Itraconazole pia hupatikana katika mfumo wa maji wenye ujazo 10mg/ml


Namna Itraconazole inavyofanya kazi ili kutibu fangasi


Dawa hii ya Itraconazole hufanya kazi zake kwa kuzuia utemgenezaji wa ukuta wa seli ya fangasi. Itraconazole na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa homoni ergosteroli, homoni hii ni muhimu sana kwani huhusika katika utengenezaji wa vijenzi muhimu vya ukita wa seli ya fangasi.


Ufyoonwaji na utoaji taka za itaconazole mwilini


Mara baada ya kutumia kwa kunywa, asilimia 55 ya dawa huingia kwenye damu endapo itatumika pamoja na chakula Dawa hii inapoingia mwilini, huvunjwa na ini kutengeneza kemikali mbalimbali na kisha kutoka kwa njia mbalimbali Asilimia 3 hadi 18 hutoka mwilini kupitia kinyesi na asilimi 40 hutolewa kwa njia ya mkojo


Dawa zilizo kundi moja na Itraconazole


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo; • Amphotericin B • Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Econazole • Flucytosine • Griseofulvin • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole


Kazi za Itraconazole


Hutumika kwenye matibabu maradhi ya fangasi wa ndani na nje ya mapafu kama vile blastomycosis, histoplasmosis na onychomycosis.


Dawa zisizopaswa kutumika na Itraconazole


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo; • Alfuzosin • Avanafil • Conivaptan • Dihydroergotamine • Dihydroergotamine intranasal • Disopyramide • Dofetilide • Dronedarone • Eliglustat • Eplerenone • Ergotamine • Estazolam • Felodipine • Fesoterodine • Flibanserin • Indapamide • Irinotecan • Irinotecan liposomal • Ivabradine • Lomitapide • Lovastatin • Lurasidone • Methadone • Methylergonovine • Midazolam • Naloxegol • Nisoldipine • Pimozide • Quinidine • Ranolazine • Silodosin • Simvastatin • Solifenacin • Ticagrelor • Tolvaptan • Triazolam • Venetoclax


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Itraconazole


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao; • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi • Wagonjwa wenye shida ya magonjwa ya Moyo kuferi


Upekee wa Itraconazole


Dawa hii nusu ya maisha yake ni masaa 21 na pia hutolewa mwili kwa njia ya mkojo kwa asilimia 40 na kwa njia ya kinyesi kwa asilimia 3-18.


Matumizi ya Itraconazole kwa mama mjamzito


Takwimu hazijaonyesha kuwa ina madhara kwa mama mjamzito. Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito


Matumizi ya Itraconazole kwa mama anayenyonyesha


Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mama ila hushauriwa itumike kwa uangalifu mkubwa kwa wanaonyonyesha

Maudhi ya Itraconazole


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Kichefuchefu • Kutapika • Kuhisi kuungua • Kuwashwa mwili • Mwili kupata Homa • Shinikizo la juu la damu • Maumivu ya tumbo • Choo kuwa kigumu


Je kama umesahau dozi yako ufanyaje?


Kama umesahau tumia dozi yako, tumia mara utakapokumbuka na kama muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

Drugbank. Itraconazole. https://go.drugbank.com/drugs/DB01167. Imechukuliwa 12/09/2021.

Mediscape. itraconazole (Rx). https://reference.medscape.com/drug/sporanox-omnel-itraconazole-342591. Imechukuliwa 12/09/2021.

FDA. Itraconazole. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2010/022484s000lbl.pdf. Imechukuliwa 12/09/2021.

FDA. SPORANOX® (itraconazole). https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2018/020083s062lbl.pdf. Imechukuliwa 12/09/2021.
bottom of page