Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Agosti 2020, 17:28:42
Dawa ya Luliconazole
Luliconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la luzu
Fomu ya dawa Luliconazole
Luliconazole kwenye fomu ya krimu yenye asilimia 1 ya kiini cha dawa
Namna Luliconazole inavyofanya kazi yake
Dawa ya Luliconazole ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na homoni ergosteroli iliyo kwenye ukuta wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matobo na kufanya ukuta wa seli kuwa na udhaifu kufa kwake
Dawa za fangasi sawa na Luliconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Econazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Miconazole
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Kazi ya Luliconazole
Hutumika katika kutibu maradhi ya fangasi inayosababishwa na tinea pedis , Versicolour ,corporis na crusis
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Luliconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Utofauti Luliconazole na dawa zingine za fangasi
Dawa hii hufikia kilele baada ya masaa 21 baada ya kutumika mwilini
Matumizi ya Luliconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi ya Luliconazole kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya Luliconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na
Ngozi kuungua
Ngozi kuwasha
Kutokwa na vipele
Je endapo utasahau dozi yako ya Luliconazole ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-