top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

2 Desemba 2020, 10:50:25

Dawa ya Nitrofurantoin

Dawa ya Nitrofurantoin

Ni dawa mojawapo ya kutibu maambukizi ya bakteria na hutumika sana kwa wajawazito kutibu UTI isiyo sugu kwa kuwa imeonekana haina madhara. Dawa hii ipo katika kundi la dawa linaloitwa. Zamani ilikuwa imewekwa kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito.


Jina jingine la dawa hii


Majina mengine ya kibiashara ya dawa hii ni Furadantin, Macrobid, Macrodantin na Nitro Macro


Dawa hii hupatikana katika fomu ya


Kimiminika na


Tembe


Tembe huwa na uzito wa


Miligramu 50 hadi 100


Namna dawa inavyofanya kazi


Hufanya kazi kwa kuzuia shughuli za kimetaboliki ndani ya seli ya bakteria kwa kuzuia mzunguko wa citric acid na uzalishaji wa vinasaba vya bakteria (DNA na RNA) ya bakteria na hivyo kufanya bakteria afe


Ufyonzaji wa dawa


Dawa hii hufyonzwa na kufika kwenye damu kwa asilimia 38 hadi 44 tu. Endapo dawa itatumiwa pamoja na chakula itafyonzwa kwa kiasi kikubwa na kubaki muda mrefu Zaidi mwilini.


Namna dawa inavyotolewa mwilini


Dawa hii kabla ya kutolewa nje ya mwili huvunjwa na ini, asilimia 25-50 ya kiini cha dawa hutolewa kama ilivyo bila kuvunjwa na ini. Asilimia 90 ya dawa yote unayokunywa hutolewa kwa njia ya mkojo.


Dawa inadumu masaa mangapi mwilini?


Dawa hii ina uwezo wa kudumu kwa muda wa masaa 16.7 hadi 19.4 kwenye damu.


Maudhi ya dawa hii


Baadhi ya maudhi ya kutumia dawa hii ni;


  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuvurufika kwa tumbo

  • Kutoa mkojo wa njano iliyokola au nyeupe iliyopauka

  • Kupoteza hamu ya kula


Baadhi ya madhara makubwa yaanayoweza kujitokeza endapo umetumia dozi kubwa zaidi ni;


  • Kushindwa kupumua

  • Kuchoka sana

  • Homa na kutetemeka

  • Maumivu ya kifua

  • Kikohozi endelevu

  • Ganzi. Hisia za kuchomachoma kwenye miguu

  • Kuvimba kwa midomo au ulimi

  • Harara kwenye ngozi


Aina ya bakteria wanaouliwa na dawa hii ni


Bakteria aina ya gramu positive na gramu negative


Magonjwa yanayotibiwa na dawa hii


  • Dawa hii hutumika kutibu magonjwa yafuatayo kwa watu wazima na watoto

  • Maambukizi ya bakteria kwenye kibofu cha mkojo

  • Maambukizi ya bakteria kwenye njia za mkojo

  • Kujikinga na maambukizi ya bakteria kwenye kibofu cha mkojo


Watu wasiopaswa kutumia


Watu wasiopaswa kutumia dawa hii ni wale;


  • Wenye figo iliyoferi au ugonjwa wa figo

  • Kuwa na historia ya kupata manjano

  • Kuwa na aleji na dawa hii

  • Kwa watu wanaokojoa chini ya kiwango kilicho kawaida yao

  • Kama upo wiki mbili au nne za mwisho katika ujauzito(yaani kipindi cha mwezi wa tisa wa ujauzito)


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa hizi


  • Chanjo hai ya BCG

  • Chanjo hai ya kipindupindu

  • Chanjo hai ya typhoid

  • Darolutamide

  • Lasmiditan

  • Pexidartinib

  • Pretomanid

  • Selinexor


Nitrofurantoin endapo itatumika na dawa zifuatazo mgonjwa anatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu sana


  • Acalabrutinib

  • Aluminum hydroxide

  • Apalutamide

  • Bazedoxifene/conjugated estrogens

  • Bupivacaine implant

  • Calcium carbonate

  • Conjugated estrogens

  • Dawa ya kupaka ya Dapsone

  • Dawa ya kupaka ya Oxybutynin

  • Didanosine

  • Digoxin

  • Eluxadoline

  • Estradiol

  • Estrogens conjugated synthetic

  • Estropipate

  • Ethinylestradiol

  • Fostemsavir

  • Glecaprevir/pibrentasvir

  • Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate

  • Mestranol

  • Mipomersen

  • Monitor closely (35)

  • Oxybutynin

  • Oxybutynin transdermal

  • Ponatinib

  • Regorafenib

  • Safinamide

  • Sodium bicarbonate

  • Sodium citrate/citric acid

  • Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid

  • Sofosbuvir/velpatasvir

  • Stiripentol

  • Tafamidis

  • Tafamidis meglumine

  • Tetracaine

  • Trimagnesium citrate anhydrous


Matumizi ya dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipinid cha ujauzito. Kufahamu kuhusu madhara kwako au kwenye ujauzito wako wasiliana na daktari wako tafadhari


Matumizi kipindi cha ujauzito


Kama upo wiki kuanzia nne za kuelekea kipindi cha kujifungua, hupaswi kutumia dawa hii. Wasiliana na daktari wako kuhusu dawa unayopaswa kutumia kipindi hiki.


Matumizi wakati wa kunyonyesha


Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kutumika wakati wa kunyonyesha endapo kwa mtoto amabaye ana umri Zaidi ya mwezi mmoja na hana matatizo ya damu ikiwa pamoja na ugonjwa wa G6PD. Hata hivyo Hakuna tafiti ambayo imeonuyesha kutokea kwa madhara yaliyoripotiwa kwa watoto walio kuwa kwenye kihatarishi yaani kuwa chini ya umri wa siku 8. Utumiaji wa dawa hii kwa wamama wanaonyonyesha inabaki kuwa uchaguzi wa daktari na matumizi ya dawa hii yasiwe sababu ya mama kuacha kunyonyesha mtoto.


Endapo umesahau kutumia dozi ufanyaje?


Endapo umesahau kutumia dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, usinywe endapo muda wa kunywa dozi ingine umekaribia kama utakavyoshauriwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023, 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.com. nitrofurantoin. https://www.drugs.com/nitrofurantoin.html. Imechukuliwa 28.11.2020

2.Drugbank. Nitrofurantoin. https://go.drugbank.com/drugs/DB00698. Imechukuliwa 28.11.2020

3.Medline plus Nitrofurantoin. https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682291.html. Imechukuliwa 28.11.2020

4.RX wiki. Nitrofurantoin. https://www.rxwiki.com/rxnorm-atc/nitrofuran-derivatives. Imechukuliwa 28.11.2020

5.Jamie Zao, Gideon Koren etal. Using nitrofurantoin while breastfeeding a newborn. Nitrofurantoin in breastfeeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4055319/. Imechukuliwa 28.11.2020

6.Summary of Use during Lactation. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK501053/. Imechukuliwa 28.11.2020

7.Web MD. Nitrofurantoin Capsule. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-14274-59/nitrofurantoin-oral/nitrofurantoin-oral/details. Imechukuliwa 28.11.2020

8.Mediscape. Nitrofurantoin (Rx). https://reference.medscape.com/drug/macrobid-macrodantin-nitrofurantoin-342567. Imechukuliwa 28.11.2020
bottom of page