Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020, 06:50:11
Dawa ya Rolitetracyxline
Rolitetracyxline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.
Fomu ya dawa
Rolitetracyxline hupatikana katika mfumo wa unga ambao hutumika kwa ajili ya maandalizi ya sindano
Namna dawa inavyofanya kazi
Dawa jamii ya Rolitetracyxline ikiwa pamoja na tetracycline hufanya kazi Ifuatayo kupambana na bakteria
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini muhimu za bakteria
Dawa zilizo kundi moja na Rolitetracyxline
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Rolitetracyxline ni;
Choltetracycline
Oxytetracycline
Demexlocycline
Doxycycline
Minocycline
Methacyxline
Tetracycline
Kazi ya dawa :
Hutumika kama mbadala wa dawa za aina ya tetracycline pale ambapo mgonjwa hawezi kumeza dawa hivyo hupewa kama sindano
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Rolitetracyxline
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acitretin
Flibanserin
Lomitapide
Tretinoin
flibanserin
lomitapide
tretinoin
Aluminum hydroxide
Aminolevulinic acid
Amoxicillin
Ampicillin
Apalutamide
Atracurium
Avapritinib
Axitinib
Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa hii
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline
Wagonjwa wa ini
Matumizi kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa hivyo inaweza kutolewa kwa mjamzito kwa tahadhari
Maudhi ya dawa
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kutapika
Kuvimba mdomo
Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-