Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Juni 2020, 05:53:22
Dawa ya Terazosin
Terazosin
Terazosin ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha Risepta Antagonisti. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Hytrin
Rangi ya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.
Terazosin inapaswa kutumiwa pamoja au pasipo na chakula mara moja kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari.
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa tembe katika milligram zifuatazo;
• 1 Mg
• 2 Mg
• 5 Mg
• 10 Mg
Namna dawa inavyofanya kazi;
Dawa jamii ya Apha Risepta Antagonisti ikiwa pamoja na Terazosin hufanya kazi zifuatazo;
• Hufunga milango ya seli yenye jina la Alpha adrenorisepta na kupelekea kulegeza na kupanua kipenyo cha mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo kubwa.
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Alpha Risepta Antagonisti) na dawa hii ni;
• Phentolamine
• Phenoxybenzamine
• Prazosin
• Doxazosin
• Alfuzosin
• Tamsulosin
• Indoramin
• Urapidil
• Bunazosin
Kazi ya dawa
• Hutumika kwa ajili ya kushusha shinikizo la juu la damu na kuwa sawa
• Hutumika kutoa nafuu kwa wagonjwa wenye uvimbe wa tezi dume kwa kusinyaza misuli ya kibofu cha mkojo na tezi dume kwa ajili ya kuwasaidia kupunguza dalili za kukojoa kwa shida
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Alpha Risepta Antagonisti)
• Dawa hii ni imara zaidi katika kundi hili ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
• Lofexidine
• Sildenafil
• Tamsulosin
• Vardenafil
• Yohimbe
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Alpha Risepta Antagonisti
Tahadhari ya dawa hii
Dozi ya kwanza ya dawa hii huweza kupelekea kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wa saratani ya tezi dume
Kundi la dawa wakati wa ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama hinaweza kuingia kwenye maziwa baada ya mama kutumia dawa hii
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
• Kizunguzungu
• Maumivu ya misuli
• Haipotension
• Kichefuchefu
• Kuvimba
• Kuishiwa pumzi
• Kuchoka
• Kuishiwa fahamu
• Kushindwa kuwa imara katika mapenzi
Mengine yanayofanyika Mwilini
Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani saa 1, nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 9 mpaka 12
Mabaki ya dawa mwilini hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 40 na kinyesi kwa asilimia 60
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau dozi yako ya dawa unapaswa kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-