Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Aprili 2020 18:58:15
Emtricitabine (FTC)
Emtricitabine (FTC) ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI (ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTIs.
Dawa hii haitumiki kama yenyewe, huchanganywa na dawa zingine za ART kudhibiti makali ya VVU.
Kundi la dawa za NRTIs hufanya kazi ya kupunguza makali ya VVU kwa kuzuia RNA ya kirusi kujitengenezea DNA. Ili RNA itengeneze DNA inahitaji kimeng’enya kinachoitwa Reverse Transcriptase, abacavir huzuia kimeng’enya hiki na hivyo kirusi kushindwa kujuzalia.
Fomu na rangi ya dawa Emtricitabine (FTC)
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa tembe na maji maji
Rangi ya kidonge hutofautina kulingana na kampuni, inaweza kuwa nyeupe, njano mpauko, n.k
Jina jingine la Emtricitabine (FTC)
Jina jingine la dawah ii hufahamika kama Emtriva.
Dawa kundi moja na Emtricitabine (FTC)
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Emtricitabine (FTC) ni:
Zidovudine (Retrovir)
Lamivudine (Epivir)
Abacavir sulfate (Ziagen)
Didanosine (Videx)
Didanosine (Videx EC)
Stavudine (Zerit)
Emtricitabine (Emtriva)
Tenofovir disoproxil fumarate (Viread)
Kazi za Emtricitabine (FTC)
Hutumika kama dawa kwenye kundi la pili kuthibiti makali ya virusi vya UKIMWI ikiwa imeunganika na Atazanavir(ATV)
Hutumika kama dawa ya ziada kwa watu ambao hujidunga madawa ya kulevya Pamoja na dawa kama ifuatavyo;
Tenofovir (TDF) + Emtricitabine (FTC) + Atazanavir (ATV/r)
emtricitabine + tenofovir disoproxil
Emtricitabine na Tenofovir
Doravirine + Lamivudine + Tenofovir
Efavirenz + Lamivudine + Tenofovir
Lamivudine + Tenofovir
Efavirenz + Emtricitabine + Tenofovir
Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyo atakavyoelekezwa na Daktari
Dawa zisizopaswa kutumika na Emtricitabine (FTC)
Emtricitabine haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Abacavir
Acyclovir
Diclofenac
Efavirenz
Zidovudine
Nevirapine
Ibuprofen
Ganciclovir
Ribavirin
Lamivudine
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Emtricitabine (FTC)
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Waliovimba ini
Wenye homa ya ini
Wenye aleji
Wakati gani Emtricitabine (FTC) itumike kwa umakini?
Inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wagonjwa wafuatao:
Wenye magonjwa ya Ini
Dozi inapaswa kupunguzwa kwa wenye magonjwa ya figo
Watu wenye magonjwa mengine yanayoharibu kinga ya mwili kama ugonjwa wa Graves
Matumizi ya Emtricitabine (FTC) kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonyesha kuwa hakuna madhara kwa mtoto wakati wa ujauzito
Matumizi ya Emtricitabine (FTC) kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha
Maudhi ya Emtricitabine (FTC)
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na:
Kuchoka
Kuwa na homa
Maumivu ya misuli
Kichwa kuuma
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kizunguzungu
Misuli kukosa nguvu
Ndoto za kutisha
Maumivu ya tumbo
Kukohoa
Kukosa usingizi
Je endapo utasahau dozi yako ya Emtricitabine (FTC) ufanyaje ?
Dawa hii hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti VVU, endapo utasahau tumia dozi yako, unapaswa tumia na Kuendelea na muda huo siku inayofuata.
Lakini ukikumbuka kunywa baada ya masaa 24 kupita, kunywa dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari na achana na dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:34:06
Rejea za mada hii:-