Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
2 Mei 2020 20:34:16
Eprosartan
Eprosartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini II Risepta bloka (ARBs). Dawa hii huwa maarufu kwa jina Teveten
Rangi ya Eprosartan
Rangi ya dawa hii ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza
Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Dozi utakayopewa itategemea hali yako ya kiafya na jinsi mwili unavyokubali matibabu
Ili kukumbuka dozi yako, tumia muda ule ule wa kunywa dawa yako kila siku. Ni muhimu kuendelea kutumia dawa hii hata kama unajisikia vizuri baada ya kuanza kutumia dawah ii.
Fomu ya Eprosartan
Eprosartan hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;
400mg
600mg
Ufanyaji kazi wa Eprosartan
Namna dawa inavyofanya kazi ili kupunguza shinikizo la damu
Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Eprosartan hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;
Hufanya kazi kwa kufunga risepta za Angiotensin II zinazojulikana kwa jina la AT1 Risepta. Risepta hizi hupatikana kwenye moyo,mishipa ya damu na figo. Risepta hizi zinapofungwa hupelekea kutanuka kwa mishipa ya damu hivyo kuwa na kipenyo kikubwa na matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.
Hupinga uzalishwaji wa homoni ya Aldosterone ambayo hutumika kuthibiti kiasi cha sodium na maji. Kiasi cha sodiamu kinapothibitiwa huweza kupunguza shinikizo la damu kwa hutanua kipenyo cha mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo la juu.
Dawa kundi moja na Eprosartan
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Azilsartan
Olmesartan
Candesartan
Irbesartan
Losartan
Telmisartan
Kazi ya Eprosartan
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu
Dawa zisizopaswa kutumika na Eprosartan
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Benazepril
Captopril
Enalapril
Fosinopril
Lisinopril
Lithium
Lofexidine
Moexipril
Perindopril
Potassium Phosphate IV
Quinapril
Ramipril
Trandolapril
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao ;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa jamii ya ARBs pia haipaswi kutumika pamoja na dawa ya Aliskiren kwa wagonjwa wa kisukari
Tahadhali kwa watumiaji wa Eprosartan
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye historia ya angioedema
Wagonjwa wenye Haipotension
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye haipovolemia
Matumizi ya Eprosartan mama mjamzito
Dawa hii inapaswa kutumika katika hali ya dharura tu pale ambapo hakuna dawa, mama akitumia dawah ii hweza kusababisha madhara kwa mtoto ambayo ni haipotension,figo kuferi na kifo
Matumizi ya Eprosartan kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu huingia kwenye kwenye maziwa.
Maudhi ya Eprosartan
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Maambukizi ya juu ya mfumo wa upumuaji
Kukohoa
Haipaglycemia
Maumivu ya mgongo
Maumivu ya tumbo
Maumivu kwenye misuli
Kuchoka
Kichefuchefu
Neutropenia
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:34:24
Rejea za mada hii:-