Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Mei 2020, 19:56:30
Erythromycin
Erythromycin yenye jina jingine la ery-ped, ni dawa jamii ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria iliyo kwenye kundi la macrolide inayozalishwa kutokwa kwa bakteria anayeitwa Saccharopolyspora erythraea.
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge, tembe na kimiminika kwa ajili ya kunywa au kimininika kwa ajili ya kutumika kwa kuchoma sindano.
Tembe ya erythromycin huwa na uzito wa miligramu 250 au 500
Ili kuzuia usugu wa dawa dhidi ya bakteria, dawa hii inatakiwa tumika kwenye matibabu yanayosababishwa na bakteria tu.
Ufyonzwaji wa dawa
Mara baada ya kunywa dawa, dawa hii hufyonzwa kwa kiasi kizuri na kuingia kwenye mfumo wa damu.
Utoaji taka mwilini
Nusu maisha ya dawa ni masaa 68, dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na kinyesi
Mwingiliano wa dawa na dawa zingine
Kutumia dawa hii pamoja na Efavirenz au fluconazole huleta mwingiliano wa wastani. Dawa ya nelfinavir huongeza kiwango cha dawa hii kwenye damu.
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na erythromycin
Afatinib
Alitretinoin
Almotriptan
Alosetron
Alprazolam
Aminolevulinic ya kupaka
Amiodarone
Amitriptyline
Amobarbital
Amoxapine
Antithrombin alfa
Antithrombin III
Apalutamide
Aprepitant
Argatroban
Aripiprazole
Armodafinil
Arsenic trioxide
Artemether/lumefantrine
Atazanavir
Atorvastatin
Avapritinib
Axitinib
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Chanjo hai ya BCG
Bemiparin
Bivalirudin
Bosentan
Bosutinib
Budesonide
Buspirone
Butabarbital
Butalbital
Carbamazepine
Chlorpromazine
Cilostazol
Cimetidine
Cinacalcet
Clarithromycin
Clobetasone
Clomipramine
Clopidogrel
Clozapine
Cobicistat
Cobimetinib
Colchicine
Conivaptan
Conjugated estrogens
Conjugated estrogens ya kuweka ukeni
Cortisone
Cyclosporine
Dalteparin
Darifenacin
Darunavir
Dasatinib
Desipramine
Dexamethasone
Dhea, herbal
Diazepam
Digoxin
Dihydroergotamine
Dihydroergotamine ya kuweka puani
Diltiazem
Disopyramide
Dofetilide
Doxepin
Dronedarone
Droperidol
Duloxetine
Edoxaban
Efavirenz
Elagolix
Eletriptan
Eliglustat
Eluxadoline
Encorafenib
Enoxaparin
Entrectinib
Epinephrine
Epinephrine racemic
Erdafitinib
Ergotamine
Eribulin
Erlotinib
Eslicarbazepine acetate
Estradiol
Estrogens conjugated synthetic
Estrogens esterified
Estropipate
Ethotoin
Etonogestrel
Etravirine
Eucalyptus
Everolimus
Felodipine
Fentanyl
Fentanyl
Fesoterodine
Flibanserin
Fluconazole
Fludrocortisone
Fluphenazine
Fondaparinux
Formoterol
Fosamprenavir
Fosphenytoin
Glasdegib
Grapefruit
Griseofulvin
Haloperidol
Heparin
Hydrocortisone
Hydroxychloroquine sulfate
Hydroxyprogesterone caproate
Ibutilide
Idelalisib
Iloperidone
Imipramine
Indapamide
Indinavir
Inotuzumab
Irinotecan
Irinotecan liposomal
Isoniazid
Itraconazole
Ivabradine
Ivosidenib
Ixabepilone
Ketoconazole
Lapatinib
Lasmiditan
Lefamulin
Lemborexant
Lofepramine
Lomitapide
Lopinavir
Loratadine
Lovastatin
Lumacaftor/ivacaftor
Lumefantrine
Macimorelin
Maprotiline
Maraviroc
Marijuana
Mestranol
Methadone
Methyl aminolevulinate
Methylprednisolone
Metronidazole
Miconazole vaginal
Midazolam
Midazolam intranasal
Mizolastine
Modafinil
Moxifloxacin
Naloxegol
Nefazodone
Nelfinavir
Neratinib
Nevirapine
Nicardipine
Nifedipine
Nilotinib
Nilutamide
Nisoldipine
Nortriptyline
Octreotide
Octreotide (antidote)
Olaparib
Ondansetron
Osimertinib
Oxcarbazepine
Oxiconazole
Panobinostat
Pazopanib
Pemigatinib
Pentamidine
Pentobarbital
Perphenazine
Pexidartinib
Phenindione
Phenobarbital
Phenytoin
Pimozide
Pitavastatin
Pitolisant
Pomalidomide
Posaconazole
Prednisolone
Prednisone
Pretomanid
Primidone
Procainamide
Prochlorperazine
Promazine
Promethazine
Protamine
Protriptyline
Quetiapine
Quinidine
Quinidine
Quinupristin/dalfopristin
Ranolazine
Repaglinide
Revefenacin
Rifabutin
Rifampin
Rifapentine
Rimegepant
Riociguat
Ritonavir
Romidepsin
Rufinamide
Saquinavir
Secobarbital
Selumetinib
Silodosin
Simeprevir
Simvastatin
Siponimod
Sirolimus
Solifenacin
Sotalol
St john's wort
Sunitinib
Tacrolimus
Tadalafil
Tazemetostat
Temsirolimus
Theophylline
Thioridazine
Tipranavir
Tizanidine
Tolterodine
Tolvaptan
Topiramate
Topotecan
Toremifene
Trazodone
Triamcinolone acetonide
Triazolam
Trifluoperazine
Trimipramine
Tucatinib
Typhoid vaccine live
Umeclidinium bromide
Vandetanib
Vardenafil
Vemurafenib
Venetoclax
Verapamil
Vilanterol/fluticasone furoate
Vilazodone
Voriconazole
Voxelotor
Warfarin
Zafirlukast
Ziprasidone
Namna dawa inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia kutengenezwa kwa vijenzi muhimu vya bakteria. Hufanya hivyo kwa kupinga utendaji kazi wa vinasaba vya bakteria.
Matumizi ya dawa
Matumizi ya dawa hii ni kwenye matibabu yaliyoosababishwa na bakteria wafuatao’
Bakteria Gram-positive
Corynebacterium diphtheria
Corynebacterium minutissimum
Listeria monocytogenes
Staphylococcus aureus
Streptococcus pneumoniae
Streptococcus pyogenes
Viridans group streptococci
Bakteria gram-negative
Bordetella pertussis
Haemophilus influenzae
Legionella pneumophila
Neisseria gonorrhoeae
Moraxella catarrhalis
Bakteria wa anaerobiki
Peptostreptococcus species
Prevotella bivia
Bakteria wengine
Chlamydia trachomatis
Entamoeba histolytica
Mycoplasma pneumonia
Treponema pallidum
Ureaplasma urealyticum
Magonjwa yanayotibiwa na Erythromycin
Maambukizi ya mfumo upumuaji yaliyosababishwa na bakteria
Listeriosisi
Nimonia iliyosababishwa na mycoplasma pneumonia
Maambukizi kwenye ngozi ya kiasi na wastani
Donda koo
Maambukizi ya patusisi
Erythrasma
PID iliyosababishwa na Neisserian gonorrhoeae
Amiba
Konjaktivaitizi iliyosababishwa na chlamydia trachomatis
Urethraitiz isiyosababishwa na gonococal endapo dawa ya tetracycline haipaswi kutumika
Kaswende
Ugonjwa wa Legionnaires
Chanjo dhidi ya homa ya rheumatiki kwa wagonjwa wa moyo
Usitumie dawa hii endapo
Una mzio na dawa hii au dawa zingine jamii ya macrolide au ketolide pia haipaswi kutumiwa pamoja na dawa hizi terfenadine, astemizole, cisapride, pimozide, ergotamine, au dihydroergotamine’
Tahadhari
Husababisha mzio
Huongeza muda wa QT kwenye moyo
Huwa sumu kwenye ini- endapo dalili za hepataitiz zinatokea acha mara moja kuendelea na dozi ya dawa hii. Dalili ni manjano, kuferi kwa ini na nekrosisi kwenye ini.
Tumia kwenye matibabu ya nimonia iliyosababishwa na bakteria aina ya Chlamydia pneumoniae, Haemophilus influenzae, Mycoplasma pneumoniae au Streptococcus pneumonia
Hupelekea kuharisha kutokana na maambukizi ya clostridium deficile
Haiingii kwa kiwango cha kutosha kwa motto ili kumkinga na kisonono
Taarifa muhimu kwa mgonjwa
Dawa hii inaweza kutumiwa pamoja au pasipo chakula. Unapotumia dawa hii hakikisha hautumii sambamba na dawa za kupunguza uzalishaji tindikali jamii ya aluminium na magneziamu.
Matumizi wakati wa ujauzito
Hakuna tafiti za kutosha kuhusu madhara wakati wa ujauzito kwa kichanga. Itumike kwa tahadhari endapo inahitajika.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama hivyo tahadhari inatakiwa kuchukuliwa endapo dawa hii itatumika kwa mama anayenyonyesha.
Matumizi kwa wazee
Matumizi kwa wazee wenye madhaifu ya ufanyaji kazi wa figo huweza kupelekea tatizo la utosikia vizuri kwa kuharibu mfumo wa fahami wa sikio.
Maudhi
Maudhi madogo ya Erythromycin ni;
Kuhisi mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Maumivu ya kifua
Tumbo kujaa gesi\kujamba
Kutapika
Choo cheusi
Manjano ya kolestatiki
Miwasho ukeni
Nefraitizi
Monilia
Maumivu ya kichwa, kizunguzungu
Kuhisi vitu vinazunguka
Huzuniko
Ichovu
Harara kwenye ngozi
Kuongezeka hisia za macho kwenye mwanga na
Angioidima
Endapo umesahau kunywa dozi yako ufanyaje?
Endapo umesahau kunywa dozi yako, kunywa pale unapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi inayofuata umekaribia sana. Endapo dozi nyingine imekaribia sana acha dozi uliyosahau kisha endelea na dozi ambayo inafuata kama ulivyoelekezwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-