Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Aprili 2020 19:27:41
Exenatide
Utangulizi
Exenatide ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la dawa linalojulikana kama Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Byetta hupatikana kwakwenye mfumo wa maji na hutumika kwa kuchoma sindano chini kidogo ya Ngozi.
Mgonjwa anayetumia dawa hii anapaswa kuwa amekula ili kuepuka madhara ya kushuka kwa sukari kwenye damu.
Exenatide hupatikana kwenye uzito wa miligramu
• 250mcg/mL
• 250mcg/mL
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Exenatide ni;
• Liraglutide
• Taspoglutide
• Lixisenatide
• Semaglutide
• Dulaglutide
Namna inavyofanya kazi;
Hufanya kazi ya kuchochea tezi kongosho kuzalisha homoni ya Insulin, hufanya kazi endapo kiwango cha sukari ni kikubwa kwenye damu.
Homoni ya Insulin husaidia seli za mwili zitumie sukari na kuhifadhi katika ini sukari inayozidi. homoni ya insulin inapozalishwa kwa wingi kutokana na shinikizo la dawah ii hupelekea kiwango cha sukari kupungua kwenye damu.
Dawa hii pia hufanya kazi ya kupuguza uzalishaji wa homoni ya glukagoni inayofanya kazi ya kuzalisha sukari kutoka kwenye ini.
Hata hivyo dawa ya Exenatide hupunguza uwezo wa tumbo kuruhusu chakula kwenda kwenye utumbo. Haya yote huchangia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.
Kazi za dawa hii ;
• Hutumika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili. Huweza kutumika yenyewe au Pamoja na dawa za Sulphonylurea au Biguanides.
Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;
• Glimepiride
• Fosinopril
• Fosamprenavir
• Fludrocortisone
• Etonogestrel
• Ethinylestradiol
• Estropipate
• Estradiol
• Eprosartan
• Enalapril
• Drospirenone
• Dexamethasone
• Desogestrel
• Darunavir
• Cortisone
• Clozapine
• Cinnamon
• Chlorthalidone
• Chlorpropamide
• Chlorothiazide
• Captopril
• Candesartan
• Betamethasone
• Benazepril
• Bbazedoxifene
• Azilsartan
• Asenapine
• Aripiprazole
• Acetaminophen
• acarbose
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Kwa wagonjwa wenye saratani ya tezi thairoidi au kuwa na historia ya saratani hii kwandugu wat umbo moja.
Wagonjwa wenye matatizo ya figo
Tahadhari ya dawa hii;
• Haitumiwi kama mbadala wa dawa homoni Insulin
• Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari aina ya 1
• Huleta hatari ya kupata pankreataitizi
• Hatari ya kufanya figo iferi kufanya kazi
• Hatari ya kupunguza uzito wa mwili haswa kwa wazee
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito kutokana na makundi yaliyowekwa na shirika la dawa la Australia.
Shirika la dawa ulimwenguni bado halijaweka dawa hii kwenye makundi ya dawa salama kipindi cha ujauzito.
Tafiti za zilizotumika kwa Wanyama zinaonyesha kuwa matumizi ya dawa hii wakati wa ujauzito huambatana na madhara makubwa ya kufisha wakati wa ujauzito. Dawa hii hupunguza ukuaji na kukomaa kwa mifupa ya mtoto akiwa tumboni, hii ni kutokana na tafiti zilizo fanyika kwa panya.
Hivyo Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito na kwa mama anayenyonyesha. Itumike tu endapo faida ni kubwa kuliko madhara ya dawa.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
• Kupata uvimbe maeneo uliyochoma sindano ya dawa hii
• Kichefuchefu
• Kutapika
• Kuharisha
• Choo kuwa kigumu
• Maumivu ya kichwa
• Kizunguzungu
• Maumivu ya misuli
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau dozi yako, tumia pale unapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umefika. Endapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana kufika acha dozi uliyosahau kisha endelea na dozi kama ulivyopangiwa na daktarin wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 10:55:40
Rejea za mada hii:-