top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

4 Mei 2020, 23:22:15

Famotidine

Famotidine

Famotidine ni dawa ambayo huzia tindikali isizalishwe kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zinazoitwa gastrini. Dawa hii iliyopo kwenye kundi la dawa zinazozuia H2 risepta antagonisti, huzuia kemikali ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni isishiriki katika kazi hiyo.


Hivyo dawa hii hutumika kutibu matatizo mbalimbali yanayotokana na tindikali ya tumboni.


Majina ya kibishara ya Famotidine


  • Pepcid

  • Famotidinum

  • Brolin

  • Gastro

  • Apogastine

  • Gastrodomina

  • Gastrosidin


Fomula ya kikemikali


  • Famotidine hufahamika kikemikali kama C8H15N7O2S3


Jina la kisayansi (IUPAC) la Famotidine


3-[[2-(diaminomethylideneamino)-1,3-thiazol-4-yl]methylsulfanyl]-N'-sulfamoylpropanimidamide


Famotidine hutibu nini?


  • Matibabu ya vidonda vya tumbo

  • Matibabu ya Kiungulia

  • Matibabu ya Kucheua tindikali

  • Kutibu michubuko kwenye koo la chakula vilivyo sababishwa na michubuko ya tindikali (kiungulia).

  • Husaidia kuzuia damu kuvuja kwenye njia ya juu ya mfumo wa chakula

  • Hutumiwa wakati mgonjwa akipewa dawa ya usingii kwa dharura ili kuzuia mgonjwa asipaliwe na tindikali kutoka tumboni


Kutibu sindromu ya Zollinger-Ellison


Dozi za Famotidine


Vidonge

  • Miligramu 10

  • Miligramu 20

  • Miligramu 40


Dawa ya kimiminika

  • Miligramu 40 kwa mililita 5


Dawa ya kuchoma kwa sindano

  • Miligramu 10 kwa mililita

  • Miligramu 0.4 kwa mililita


Namna ya kutumia Famotidine


  • Tumia kama utakavyo elekezwa na daktari.

  • Matumizi yanategemea ni hali gani inatibiwa na hali ya mgonjwa.

  • Dawa hii inaweza kutumiwa pamoja na au bila chakula.


Namna Famotidine inavyofanya kazi mwilini


  • Dawa hii huzuia risepta za H2 kupokea homon ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni

  • Kwa kufanya hivyo dawa hii huzuia utengenezaji wa tindikali tumboni na hivyo kusaidia kutibu magonjwa na hali mbalimbali kutokana na uzalishaji wa tindikali ya tumboni.


Mwili unachofanya kwa Famotidine


  • Asilimi 45 tu ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye damu baada ya kumeza dawa.

  • Huanza kufanya kazi kati ya saa 1 hadi 4 baada ya kumezwa.

  • Hufanya kazi mwilini kwa saa10 hadi 12.

  • Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondolewa sumu.

  • Sehemu kubwa ya taka mwili ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo.


Maudhi madogo madogo ya famotidine


  • Maumivu ya kichwa

  • Kizunguzungu

  • Kutopata choo

  • Homa

  • Mwili kufa ganzi

  • Kuchoka

  • Kuwashwa

  • Mdomo kukauka

  • Kichefuchefu

  • Tumbo kuuma

  • Kuchanganyikiwa hususani kwa wazee.

  • Mara chache inaweza kupunguza uwezo wa kufanya tendo kwa wanaume.


Famotidine marufuku kutumika kwa


Wagonjwa wenye aleji na dawa ya fomatidine.


Tahadhari wakati wakutumia fomatidine


Matumizi ya fomatidine kwa wazee na wenye shida ya figo dawa hii inaweza kusababisha yafuatayo;


  • Kuchanganyikiwa

  • Kuona maruweruwe

  • Kupata degedge

  • Mwili kukosa nguvu


Kwa wagonjwa wenye saratani ya tumbo, kupata nafuu wakati antumia dawah ii haimaanishi kua saratani imetibka.


Muingiliano na dawa nyingine


Famotidine isitumike pamoja na dawa zifuatazo kwani huzuia ufyonzwaji wa dawa hizo;


  • Dasatinib

  • Delavirdine mesylate

  • Cefditoren

  • Fosamprenavir

  • Ikitumika pamoja na tizanidine ina weza kusababisha shinikizo la la damu kushuka, mapigo ya moyo kuwa taratibu na mwili kukosa nguvu


Dawa zifuatozo hupunguza ufyonzwaji wa famotidine:


  • Sodium bicarbonate

  • Calcium carbonate

  • Magnesium dihydroxide

  • Magnesium carbonate

  • Magnesium trisilicate

  • Aluminium hydroxide

  • Metoclopramide


Matumizi ya Famotidine wakati wa ujauzito


Ni vyema kuepuka matumizi ya Famotidine wakati wa ujauzito kwa hakuna taarifa/tafiti za kutosha juu ya madhara yake kwa mtoto aliyeko tumboni wakati wa ujauzito. Ikibidi kutumia dawa hii basi uzito wa faida kwa mama na madhara kwa mtoto unabidi uzingatiwe.


Matumizi ya Famotidine wakati wa kunyonyesha


Pia ni vyema kuepuka matumizi ya dawa hii wakati wa kunyonyesha kwani hufika kwenye maziwa ya mama na inaweza kusababisha madhara kwa mtoto anaenyonya. Daktari anaweza kutumia dawa nyingine zenye manufaa zaidi na ikilazimu kutumia famotidine basi uzito wa faida kwa mama na madhara kwa mtoto unabidi uzingatiwe. Moja ya njia ya kutatua utata kama huu ni mtoto kuachishwa kunyonya kama mama atatumia dawa ya kumdhuru mtoto anaye nyonya.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023, 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of THERAPEUTICS twelfth edition ISBN: 978-0-07-176939-6 ukurasa wa 1313.

2.Pub chem: https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Famotidine imechukuliwa 01/05/2020.

3.U.S. Food and Drug Administration:
https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2018/019462s039lbl.pdf imechukuliwa 01/05/2020.
bottom of page