top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

28 Aprili 2020, 18:04:38

Gliquidone

Gliquidone

Gliquidone ni dawa mojawapo inayotumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa kisukari iliyo kwenye kundi la sulfonylurea kizazi cha pili. Dawa hii inaweza kusababisha mgonjwa akakojoa mara kwa mara.


Majina ya kibiashara ya Gliquidone


  • Glurenorm

  • Beglynor

  • Gliquidonum


Fomula ya kikemikali


Fomu ay kikemikali ya Gliquidone ni C27H33N3O6S


Jina la kisayansi (IUPAC)


Gliquidone hufahamika kama 1-cyclohexyl-3-[4-[2-(7-methoxy-4,4-dimethyl-1,3-dioxoisoquinolin-2-yl)ethyl]phenyl]sulfonylurea


Namna ya kutumia Gliquidone


  • Meza kama ulivyo elekezwa na daktari wako.

  • Dawa hii huweza kutumika pamoja na dawa nyingine kama vile metformin kama akipendekeza daktari wako.

  • Dawa za kushusha sukari hutumika sambamba na lishe Pamoja na mazoezi sahihi kwa wagonjwa wa kisukari.


Ufanyaji kazi wa Gliquidone


Inachochea seli beta za kongosho kuzalisha insulini ambayo ndiyo hushusha sukari ya damu.

Inapunguza kasi ya ini kutengeneza sukari.


Muingiliano na dawa zingine


Dawa zinazoongeza ufanisi wa gliquidone;

  • Chloramphenicol

  • Clofibrate

  • Fluconazole

  • Methyldopa

  • Isocarboxazid

  • Phenelzine

  • Tranylcypromine

  • Choline salicylate

  • Diflunisal

  • Magnesium salicylate

  • Salsalate

  • Sodium salicylate

  • Sodium thiosalicylate

  • Sulfamethizole

  • Sulfamethoxazole

  • Sulfasalazine

  • Sulfisoxazole

  • Trimethoprim

  • Trimethoprim–sulfamethoxazole

  • Trisulfapyrimidine

  • Trovafloxacin


Dawa zinazo punguza ufanisi wa Gliquidone

  • Vidonge vya uzazi wa mpango

  • Amlodipine

  • Bepridil

  • Diltiazem

  • Nicardipine

  • Nifedipine

  • Verapamil

  • betamethasone

  • budesonide

  • dexamethasone

  • Dexone,

  • hydrocortisone

  • sodium phosphate


Nani asiyepaswa kutumia Gliquidone


Marufuku kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wagonjwa wenye aleji na kemikali zenye salfa.

  • Wagonjwa wa wa kisukari aina ya kwanza


Maudhi madogo ya Gliquidone


  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kichwa

  • Kichefuchefu

  • Kuwashwa ngozi

  • Kuharisha

  • Maumivu ya tumbo


Madhara makubwa ya Gliquidone


  • Sukari kushuka kupita kiasi

  • Kupoteza fahamu

  • Mzio mkali wa sindromu ya Steven Johnson


Matumizi ya Gliquidone wakati wa ujauzito na kunyonyesha


Ni vyema kuepuka kutumia dawa hii wakati wa ujauzito na kunyonyesha kwani hakuna taarifa za kutosha juu ya madhara yake wakati wa ujauzito au wakati wa kunyonyesha. Dawa nyingine zinazopendekezwa na mamlaka za afya kama vile insulin zinaweza kutumika.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:33:45

Rejea za mada hii:-

1.Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of THERAPEUTICS twelfth edition ISBN: 978-0-07-176939-6 ukurasa wa 1257.

2.Drug bank: https://www.drugbank.ca/drugs/DB01251 imechukuliwa 27/04/2020.

3.Pub Chem: https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/91610 imechukuliwa 27/04/2020
bottom of page