top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

31 Machi 2020, 14:45:32

Ibuprofen

Ibuprofen

Ibuprofen ni dawa jamii ya NSAIDs inayotumika kutibu maumivu kwa kuzuia mwili kutoa baadhi ya kemikali zinazosababisha homa uvimbe na maumivu.


Fomu na uzito na rangi ya dawa Ibuprofen


Dawa hii hupatikana katika fomu tofauti tofauti Kama vile


  • Vidonge vya kumeza mfano; Kidonge cha miligramu 100, 200, 400, 600 n.k

  • Tembe zenye miligramu 200

  • Vidonge vya kutafuna

  • Kimiminika mfano cha miligramu 100/ kwa lila mililita 5


Kidonge cha ibrupofeni kinaweza kuwa na rangi ya pinki, machungwa nyeupe na rangi zingine.


Ibuprofen hutibu nini?


  • Hutumika kutibu maumivu ya maungio ya mwili kama osteoarthraitizi

  • Kutuliza homa

  • Kutibu maumivu ya misuli na masikio

  • Kutibu maumivu ya hedhi

  • Kutibu maumivu ryumatoidi arthraitizi

  • Kutibu magonjwa ya inflamasheni

  • Hutumika Kama Kinga kwa ya ugonjwa wa Alzheimer's na Parkinson's kwa wazee.


Maudhi madogo ya Ibuprofen


  • Kizunguzungu

  • Maumivu kwenye epigastriamu (chembe ya moyo)

  • Kiungulia

  • Konstipesheni

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kutokwa na upele

  • Masikio kupiga kelele

  • Uvimbe

  • Mwili kujaa maji


Tahadhari kwa watumiaji wa Ibuprofen


Hatari kwenye mfumo wa moyo.

Dawa jamii ya NSAIDs ikiwemo ibuprofen huweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo na matukio ya

thrombotiki, kiharusi, infaksheni ya mayokadia na kuweza kusababisha kifo kwa binadamu.

Hatari huongezeka zaidi kutokana/ kulingana na muda wa matumizi ya dawa.

NSAIDs haziruhusiwi kutumika wakati wa upasuaji wa mishipa ya damu.


Hatari katika mfumo wa chakula.

  • Dawa jamii ya NSAIDs huweza kuongeza hatari ya damu tumboni, vidonda vya tumbo na kutoboa

  • utumbo na tumbo ambapo mtu huweza kupoteza maisha.

  • Madhara kwenye mfumo wa chakula huweza kutokea ghafra bila ishara.

  • Wazee wapo hatarini kupata madhara mabaya kwenye mfumo wa chakula.


Katazo la utumiaji wa Ibuprofen


Ni marufuku kutumia dawa hii kwa mtu mwenye mzio na dawa hii, mwenye historia ya utatu wa aspirin, kutibu wagonjwa waliofanyiwa au wanaotaka kufanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu ya moyo na koronari.


Dawa ambazo hasipaswi kutumika na Ibuprofen


Dawa hii isitumike na dawa zifuatazo;


  • Quinapril

  • Ramipril

  • Siponimod

  • Tacrolimus

  • Trandolapril

  • Aminolevulinic asidi ya kupaka au kumeza

  • Erdafitinib

  • Fosinopril

  • Ketorolac

  • Ketorolac intranasal

  • Lisinopril

  • Apixaban

  • Aspirin

  • Moexipril

  • Naproxen

  • Oxaprozin

  • Benazepril

  • Captopril

  • Enalapril

  • Methotrexate

  • Methyl aminolevulinate

  • Pemetrexed

  • Perindopril

  • Pexidartinib

  • Pretomanid


Ibuprofen itumike chini ya uangalizi endapo itatumipa pamoja na dawa zipi?

  • Ticlopidine

  • Timolol

  • Tobramycin ya kuvuta

  • Tolazamide

  • Tolbutamide

  • Tolfenamic asidi

  • Tolmetin

  • Tolvaptan

  • Torsemide

  • Trandolapril

  • Travoprost ya macho

  • Trazodone

  • Triamcinolone acetonide ya kuchoma

  • Triamterene

  • Unoprostone ya macho

  • Valsartan

  • Venlafaxine

  • Vitamin K1

  • Vorapaxar

  • Vortioxetine

  • Warfarin

  • Zanubrutinib

  • Zotepine

  • Acebutolol

  • Aceclofenac

  • Acemetacin

  • Agrimony

  • Albuterol

  • Alfalfa

  • Alfuzosin

  • Aliskiren

  • Alteplase

  • Amikacin

  • Amiloride

  • Antithrombin alfa

  • Antithrombin iii

  • Arformoterol

  • Argatroban

  • Asenapine

  • Aspirin aina yoyote

  • Atenolol

  • Clomipramine

  • Clopidogrel

  • Cordyceps

  • Cortisone

  • Cyclopenthiazide

  • Cyclosporine

  • Dabigatran

  • Dalteparin

  • Deferasirox

  • Defibrotide

  • Deflazacort

  • Dexamethasone

  • Dichlorphenamide

  • Diclofenac

  • Diflunisal

  • Digoxin

  • Dobutamine

  • Dong quai

  • Dopexamine

  • Doxazosin

  • Dronabinol

  • Drospirenone

  • Duloxetine

  • Edoxaban

  • Efavirenz

  • Eltrombopag

  • Eluxadoline

  • Elvitegravir/cobicistat/emtricitabine/tenofovir df

  • Emtricitabine

  • Enalapril

  • Enoxaparin

  • Ephedrine

  • Epinephrine

  • Epinephrine racemic

  • Epoprostenol

  • Eprosartan

  • Escitalopram

  • Esmolol

  • Ethacrynic acid

  • Etodolac

  • Fenbufen

  • Fennel

  • Fenoprofen

  • Feverfew

  • Fish oil triglycerides

  • Flucloxacillin

  • Fludrocortisone

  • Fluoxetine

  • Flurbiprofen

  • Fluvoxamine

  • Fondaparinux

  • Formoterol

  • Forskolin

  • Fosinopril

  • Furosemide

  • Garlic

  • Gemifloxacin

  • Gentamicin

  • Ginger

  • Ginkgo biloba

  • Glimepiride

  • Glipizide

  • Glyburide

  • Green tea

  • Heparin

  • Horse chestnut seed

  • Hydralazine

  • Hydrochlorothiazide

  • Hydrocortisone

  • Ibrutinib

  • Imatinib

  • Indapamide

  • Indomethacin

  • Irbesartan

  • Isoproterenol

  • Ketoprofen

  • Ketorolac

  • Ketorolac intranasal

  • Labetalol

  • Lacosamide

  • Latanoprost

  • Azficel-t

  • Azilsartan

  • Bemiparin

  • Benazepril

  • Bendroflumethiazide

  • Betaxolol

  • Betrixaban

  • Bimatoprost

  • Bisoprolol

  • Bivalirudin

  • Budesonide

  • Bumetanide

  • Candesartan

  • Captopril

  • Carbamazepine

  • Carbenoxolone

  • Carvedilol

  • Celecoxib

  • Celiprolol

  • Chlorothiazide

  • Chlorpropamide

  • Chlorthalidone

  • Choline magnesium trisalicylate

  • Cinnamon

  • Ciprofloxacin

  • Citalopram

  • Clobetasone

  • Latanoprostene bunod ophthalmic

  • Lesinurad

  • Levalbuterol

  • Levofloxacin

  • Levomilnacipran

  • Lisinopril

  • Lithium

  • Lornoxicam

  • Losartan

  • Lumacaftor/ivacaftor

  • Meclofenamate

  • Mefenamic acid

  • Melatonin

  • Meloxicam

  • Mesalamine

  • Metaproterenol

  • Methyclothiazide

  • Methylprednisolone

  • Metolazone

  • Metoprolol

  • Milnacipran

  • Mipomersen

  • Mistletoe

  • Moexipril

  • Moxifloxacin

  • Moxisylyte

  • Mycophenolate

  • Nabumetone

  • Nadolol

  • Nebivolol

  • Nefazodone

  • Nettle

  • Norepinephrine

  • Olmesartan

  • Ospemifene

  • Panax ginseng

  • Parecoxib

  • Paroxetine

  • Pau d'arco

  • Pegaspargase

  • Peginterferon alfa 2b

  • Penbutolol

  • Perindopril

  • Phenindione

  • Phenoxybenzamine

  • Phentolamine

  • Phytoestrogens

  • Pindolol

  • Pirbuterol

  • Piroxicam

  • Pivmecillinam

  • Potassium acid phosphate

  • Potassium chloride

  • Potassium citrate

  • Potassium iodide

  • Pralatrexate

  • Prasugrel

  • Prazosin

  • Prednisolone

  • Prednisone

  • Probenecid

  • Propranolol

  • Protamine

  • Quinapril

  • Ramipril

  • Reishi

  • Reteplase

  • Rivaroxaban

  • Rivastigmine

  • Sacubitril/valsartan

  • Salicylates (non-asa)

  • Salmeterol

  • Salsalate

  • Saw palmetto

  • Sertraline

  • Siberian ginseng

  • Silodosin

  • Sodium picosulfate/magnesium oxide/citric asidi isiyo na maji

  • Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate

  • Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate/polyethylene glycol

  • Sotalol

  • Spironolactone

  • Succinylcholine

  • Sulfasalazine

  • Sulindac

  • Tafluprost

  • Telmisartan

  • Temocillin

  • Tenecteplase

  • Tenofovir df

  • Terazosin

  • Terbutaline

  • Ticagrelor

  • Ticarcillin


Angalizo


Ibuprofen itumike kwa umakini kwa wagojwa wenye


  • Pumu

  • Moyo kufeli

  • Magojwa ya ini

  • Magojwa ya moyo

  • Vidonda vya tumbo

  • Tatizo ka kutokwa damu

  • Hatua ya mwisho ya mimba

  • Tatizo la presha kupanda

  • Mgonjwa wa kisukari.


Matumizi ya Ibuprofen kipindi cha Ujauzito na kunyonyesha


Matumizi ya dawa hii wakati wa ujauzito huweza kusababisha kufunga kwa daktas arteriosus kabla ya wakati.


Matumizi ya Ibuprofen kwa mama anayenyonyesha


Tafiti zinaonekana kuwa kiwango cha dawa kinachopita na kuingia katika maziwa ya mama ni kidogo Sana.


Dawa hii Ina muda mfupi wa nguvu kazi mwilini ( masaa 2-3), na inaaminika ni Salama kwa watoto wadogo na imepewa kipaumbele kwa akina mama wanaonyonyesha Kama analgesics au inflamesheni.


Jinsi ya kutumia dawa Ibuprofen


Meza dawa ukiwa umekula au kunywa maji ili kuzuia madhara kwenye mfumo wa chakula.

Usitumie dawa nje ya maelekezo uliopewa na mtaalam.

Usitumie dawa kwa muda wa zaidi ya siku 10 ila tu Kama imetokewa maelezo ya daktari.


Endapo umesahau dozi ya Ibuprofen ufanyaje?


Endao umesahau kutumia dozi yako ya Ibuprofen, kunywa pale utakapokumbuka, endapo muda wa dozi nyingine umekaribia, acha dozi uliyosahau na kunywa dozi inayofuata kisha endelea kunywa dozi yako muda huu mpya ambao umekumbuka kama ulivyoshauriwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:31:31

Rejea za mada hii:-

1.Tripathi KD. Non steroidal anti inflammatory drugs and anti pyretic analgesics. In: Essentials of medical pharmacology. 5th edn., Jaypee Brothers, New Delhi, 2003. p. 176. (Google Scholar).

2.Aycock DG. Ibuprofen: a monograph. Am. Pharm., NS 1991; 31(1):46-49. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3191627/ imechukuliwa 30.03.2020

3. Ibuprofen FDA.
bottom of page