Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Aprili 2020 17:29:09
Metformin
Ni dawa mojawapo iliyo kwenye kundi la Biguanide, hutumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii huuzwa sana/ hufahamika kwa jina la Glucophage.
Metformin ni aina ya kwanza ya dawa kugunduliwa kutibu kisukari cha aina ya pili na hufanya kazi vizuri zaidi kwa watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi
Dawa hii hutumiwa kwa kumeza kidonge na inapaswa kutumiwa mara baada ya kula chakula.
Mara nyingi rangi ya kidonge ni nyeupe lakini hata hivyo inategemea rangi ya kiwanda kinachotengeneza dawa.
Dawa zilizo kundi moja na Metformin
• Proguanil
• Buformin
• Chlorhexidine
• Phenformin
• Chlorproguanil
• Cycloguanil
Jinsi Metformin inavyofanya kazi
Hufanya kazi ya kupunguza kiasi cha sukari kinachoingia kwenye damu kutoka kwenye ini.
Huongeza matumizi ya glukosi mwilini na kuzuia isiwe nyingi kwenye damu.
Hufanya seli za beta zilizo kwenye kongosho ziitikie uzalishaji wa homoni ya Insulin. Homoni ya insulin hufanya kazi ya kupunguza kiwango cha sukari kwenye dam una kuongeza utumiaji wa sukari kwenye damu.
Kazi za dawa ya Metformin
• Hutumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili ambacho mara kinachosababishwa na uzalishaji mdogo.
• Hutumika kuzuia aina ya kisukari aina ya pili
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Metformin
• Pombe
• Loversol
• Methylene blue
• Ranolazine
• Media za contrasti
• Selegiline
• Tafenoquine
• Ttedizolid
• Tranylcypromine
Tahadhari ya Metformin kwa wagonjwa wafuatao;
• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
• Wenye moyo ulioferi
• Dayabetiki ketoasidosisi- DKA
• Kuferi kwa figo hatua za mwisho
• Kiwango kikubwa cha creatinine kwenye damu
Tahadhari ya Metformin
• Hushusha sana kiwango cha sukari haswa kwa wazee na hivyo kusababisha haipoglaisemia. Inapaswa kutumika kwa umakini
• Huweza kupelekea kuishiwa maji mwilini
• Kutokutumia Pamoja na chakula na maji wakati wa kunywa dawa hii wakati mtu anasubiri upasuaji huweza kupelekea kuishiwa maji na shinikizo la damu kuwa chini
• Huweza kuathiri ufyozwaji wa Vitamin B12
Matumizi ya Metformin Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Metformin haina shida endapo itatumika kwa mama mjamzito maana haina hatari yeyote kwa mtoto, husaidia kuzuia athari za kupelekea kifafa cha mimba.
Kwa mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonekana kuwa kuna kiwango cha dawa ya Metformin hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama hata hivyo haina madhara kwa mtoto.
Maudhi ya Metformin
• Misuli kuishiwa nguvu
• Kuharisha
• Tumbo kujaa gesi
• Udhaifu
• Maumivu ya misuli
• Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa upumuaji
• Haipoglaisemia
• Upungufu wa vitamin B-12
• Kichefuchefu
• Kutapika
• Kizunguzungu
• Tumbo kuwa kubwa
• Choo kuwa kigumu
• Kiungulia
Je endapo umesahau dozi ya Metformin ufanyeje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, unaweza kunywa mara pale utakapokumbuka. Isipokuwa kama muda umekaribia ruka dozi hiyo na endelea na dozi kama ulivyopangiwa na daktarin wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Januari 2022 19:44:56
Rejea za mada hii:-