Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
20 Aprili 2020 07:19:24
Naproxen
Ni dawa ya kutuliza maumivu makali ya mwili. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa jamii ya NSAIDS. Hupatikana mfumo wa vidonge, tembe au kimiminika
Dawa hii hufanya kazi yake kwa kuzuia uzalishwaji wa prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa husababisha homa Pamoja na uvimbe kwenye sehemu ya mwili yenye tatizo.
Umetaboliwa dawa
Umetaboli wa Dawa hii Ni hufanyika kwenye Ini na Utoaji taka mwili kupitia Figo
Uzito na fomu wa Naproxen
• Inapatikana mfumo wa kidonge milligram 250, 500
• Inpatikana kwenye mfumo wa tembe miligramu 220
• Na inapatikana kwenye mfumo wa kimiminika
Magonjwa yanayotibiwa na naproxen
Dawaya Naproxen hutumika kutibu;
• Homa Kali
• Kupunguza maumivu ya misuli, kichwa, mifupa
• Kupunguza uvimbe (kuvimba kwa mwili baada ya jeraha)
• Kutuliza maumivu ya kipada uso
• maumivu ya kichwa
• Maumivu ya misuli, misuli kukakamaa
• Maumivu wakati wa hedhi
Maudhi madogo madogo ya Dawa hii
• Kichefuchefu na kutapika
• Kuharisha
• Maumivu ya kichwa
• Kizunguzungu
• Masikio kupiga kelele
• Uchovu wa mwili
• Maumivu ya tumbo
• Kupoteza hamu ya chakula
• Kupumua kwa shida
• Upele katika ngozi
Tahadhari ya Naproxen
Wenye shida ya Ini
Wenye matatizo ya Moyo
Wenye shida ya Figo
Wenye mzio wa Naproxen au dawa zingine
Wenye vidonda vya tumbo angalizo kuwepo kwasababu matumizi ya Dawa hii hupelekea michubuko kwenye mfumo wa chakula.
Wenye pumu (asthma)
Dawa zisizopaswa kutumika na naproxen
Dawa hii hairuhusiwi kutumika pamoja na;
• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa jamii ya NSAIDS mfano aspirin, ibuprofen, naproxen hii hupelekea hatari ya kupata vidonda vya tumbo
• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa zinazozuia damu kuganda mfano warfarin
• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa jamii ya steroids mfano Prednisone
• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa digoxin
• Usitumie dawa hii pamoja na Dawa probenecid
• Usitumie dawa hii pamoja na Dawa diuretic mfano furesimide
• Usitumie dawa hii pamoja na Dawa jamii ya ACE mfano captopril, Lisinopril
Dawa zingine ambazo hazipaswi kutumika pamoja na dawa hii ni;
• Lisinopril
• Methotrexate
• Methyl aminolevulinate
• Moexipril
• Pemetrexed
• Perindopril
• Quinapril
• Ramipril
• Aminolevulinic ya kumeza
• Aminolevulinic ya kupaka
• Apixaban
• Benazepril
• Captopril
• Tacrolimus
• Trandolapril
• Enalapril
• Erdafitinib
• Fosinopril
• Ketorolac
• Siponimod
Matumizi ya Naproxen Kwa Wajawazito na wanaonyonyesha
Tahadhari wakati wa ujauzito isitumike kwa mama mjamzito haswa miezi ya mitatu mwishoni ya ujauzito.
Kwa Wanaonyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.
Je endapo umesahau dozi ya Naproxen ufanyeje?
Kama umesaau kunywa dose yako unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka, isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika, acha dozi uliyoruka na kunywa dozi ingine kwa mud auliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Januari 2022 19:27:46
Rejea za mada hii:-