top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

13 Aprili 2020, 15:04:46

Olanzapine

Olanzapine

Ni dawa ya kutibu magonjwa ya akili, iliyo kwenye kundi la antisaikotiki. Baadhi ya magonjwa hayo ni magonjwa ya schizophrenia na baipola.


Majina ya kibiashara


Olanzapine hufahamika kwa majina ya kibiashara kama;

  • Lybalvi

  • Olazax

  • Symbyax

  • Zalasta

  • Zypadhera

  • Zyprexa


Fomu ya Olanzapine


Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge na maji yanayotolewa kwa kuchomwa sindano.


Olanzapine na chakula


Haina madhara yeyote ikitumika na chakula


Dawa kundi moja na olanzapine


Dawa zilizo kundi moja na Olanzapine


  • Quetiapine

  • Risperidone

  • Aripiprazole

  • Ziprasidone


Jinsi Olanzapine inavyofanya kazi


Dawa ya olanzapine hufunga milango ya kuingilia homoni za dopamine D1, D2, D4, histamine 5-HT2 na risepta za muskariniki.


Utoaji olanzapine mwilini


Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya kinyesi na mkojo


Olanzapine hutibu nini?


  • Hutumika kutibu ugonjwa wa Schizofrenia

  • Hutumika kutibu magonjwa ya Baipola mania

  • Hutumika kutibu hali ya huzuni na sononeko(dipresheni)

  • Hutumika kuondoa hali ya kichefuchefu na kutapika inapotumika na Dexamethasone


Mwingilinao wa olanzapine na dawa zingine


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na olanzapine;


  • Apomorphine

  • Benzhydrocodone

  • Bomocriptine

  • Cabergoline

  • Dopamine

  • Entrectinib

  • Erdafitinib

  • Fedratinib

  • Fluvoxamine

  • Glasdegib

  • Hydrocodone

  • Hydroxychloroquine sulfate

  • Ivosidenib

  • Levodopa

  • Lisuride

  • Macimorelin

  • Mefloquine

  • Methyldopa

  • Ondansetron

  • Pefloxacin

  • Pitolisant

  • Pramipexole

  • Ropinirole

  • Safinamide

  • Siponimod

  • Sodium oxybate

  • Umeclidinium bromide

  • Vilanterol


Tahadhali ya olanzapine


  • Huweza kupelekea kupungua kwa kiasi cha chembechembe nyeupe za damu

  • Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye daimenshia

  • Huweza kupelekea Kiharusi

  • Huweza kuathiri uwezo wa mtu kusimama wima kwa muda mrefu

  • Huweza kuathiri mtu kuwa hali ya kuchanganyikiwa

  • Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye aleji na dawa hii


Olanzapine na ujauzito


Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito


Olanzapine kipindi cha kunyonysha


Kwa mama anayenyonyesha haipaswi kutumika kwao sababu huingia kwenye maziwa.


Maudhi ya olanzapine


  • Hupelekea hali ya kuanguka baada ya mtu kusimama kwa muda mrefu

  • Kuongezeka uzito

  • Kuwa mdhaifu

  • Kizunguzungu

  • Kukosa usingizi

  • Kukosa Choo

  • Sukari kuwa juu

  • Shinikizo la damu kushusha

  • Kutetemeka

  • Kupunguza nguvu ya misuli


Je, kama umesahau dozi ya olanzapine ufanyeje?


Kama umesahau kutumia hii dozi yako ya olanzapine, tumia pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umeakaribia sana, subiri muda ufike ndipo utumie dozi hiyo kama alivyopangiwa na daktari.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:27:49

Rejea za mada hii:-

1.BNF September 2018- march 2019, kurasa wa 394-395. bnf.org

2.Web Md.Olanzapine. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-1644-9274/olanzapine-oral/olanzapine-oral/details. Imechukuliwa 13/4/2020

3.Health Line.Olanzipine. https://www.healthline.com/health/olanzapine-oral-tablet . Imechukuliwa 13/4/2020

4.Medscape.Olanzipine. https://reference.medscape.com/drug/zyprexa-relprevv-olanzapine-342979. Imechukuliwa 13/4/2020

5.Drugbank. olanzipine. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00334. . Imechukuliwa 13/4/2020
bottom of page