Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Mei 2020 23:06:00
Omeprazole
Omeprazole ni dawa iliyopo kwenye kundi la protoni pumpu inhibita ambayo hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayotokana na kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali za tumbo.
Majina ya kibiashara
Majina mengine ya Omeprazole ni
Prilosec
Losec
Antra
Omeprazon
Audazol
Omapren
Fomula ya kikemikali ya Omeprazole
Fomula ya kikemia ya Omeprazole ni C17H19N3O3S
Jina la kisayansi la Omeprazole
Omeprazole huwa na jina la kisayansi la 6-methoxy-2-[(4-methoxy-3,5-dimethylpyridin-2-yl)methylsulfinyl]-1H-benzimidazole
Omeprazole hutibu nini?
Omeprazole hutumika yenyewe au pamoja na dawa zingine katika matibabu ya;
Vidonda vya tumbo.
Vidonda vya tumbo vinavyo sababishwa na dawa zilizopo kwenye kundi la NSAID.
Sindromu ya Zollinger-Ellison
Kupunguza ualishaji wa tindikali tumboni kabla au baada ya kufanyiwa upasuaji.
Kucheua tindikali
Kutibu michubuko ya koo la chakula kutokana na tindikali
Fomu na uzito wa Omeprazole
Kidonge cha miligramu
20 au
40
Tembe za;
Miligramu 10 (kwa watoto)
Miligramu 20
Miligramu 40
Dozi iliyo katika hali kimiminika
Miligramu 2 kwa mililita 1 (2mg/ml)
Ufanyaji kazi wa Omeprazole
Huzuia hatua za mwisho za utengenezaji wa tindikali (acid) tumboni. Hili ni muhimu katika kutibu vidonda vya tumbo na kiungulia.
Ufyonzwaji wa Omeprazole
Hufyonzwa kwa asilimia 30 hadi 40 kwenda kwenye damu baada ya kumeza
Umetaboli wa Omeprazole
Huchakatwa kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondoa sumu.
Huanza kufanya kazi saa 1 baada ya kumezwa.
Huweza kufanya kazi mwilini hadi kwa saa 73.
Nusu maisha Omeprazole
Nusu maisha ya Omeprazole kati ya saa 0.5 hadi 1.
Utoaji wa Omeprazole mwilini
Taka mwili za mabaki ya omeprazole hutolewa kwenye mkojo (asilimia 77) na kinyesi (asilimia 19).
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Omeprazole
Wagonjwa wenye aleji na omeprazole
Angalizo la omeprazole
Kuhara wakati wa mgojwa anatumia omeprazole kunaweza kusababishwa na baktreria Clostridium difficile na sio dawa.
Kutumia dawa hii kwa muda mrefu kunaweza kudhohofisha mifupa na kusababisha mifupa kuvunjika kwa urahisi.
Matumizi ya muda mrefu yanaweza kusabisha kushuka kwa kiwango cha magnesium kwenye damu.
Inaeeweza kusababisha baadhi vipomo kwenye mfumo homoni na tezi kutoa majibu yasiyo sahihi kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ChoromograninA kwenye damu.
Epuka kutumika dawa hii kwa pamoja na dawa rimfampicin kwani rimfampicin hupunguza kiwango cha omeprazole kwenye damu.
Punguza dozi ya omeprazole kwa wagonjwa wenye shida ya ini.
Muingiliano wa Omeprazole na dawa nyingine
Dawa za kupunguza makali ya VVU atazanavir na nelfinavir, kiwango chake kwenye damu hupungua kama ikitolewa pamoja na omeprazole.
Saquinavir ambayo nayo hutumikka kupunguza makali ya VVU ufyonzwaji wake huengezeka endapo ikitumika pamoja na omeprazole.
Kiwango cha dawa zifuatazo kwenye damu huongezeka pindi zikitumiwa na omeprazole;
Clopidogrel
Tacrolimus
Methotrexate
Hupunguza utendaji kazi wa dawa zifuatazo;
Ketoconazole
Itraconazole
Digoxin
Dawa za chumvi zenye madini ya chuma
Erlotinib
Dasatinib.
Kutumia dawa hii pamoja na Clarithromycin pamoja na dawa nyingine kunaweza sababisha madhara. Hivyo daktari lazima afahamu atakavyo itumia na dawa nyingine.
Kutumia kwa pamoja na dawa ya warfarin inaweza kusababisha kuvuja damu nyingi na kuhatarisha maisha. Inabidi kufuatilia muda wa prothrombini.
Omeprazole kwenye ujauzito
Dawa itumike kwa tahadhari kama faida ya kutumia ni kubwa kuliko madhara; Majaribio kwa wanyama yanaonesha madhara na majaribio kwa binadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama na kwa binadamu hayajafanyika.
Omeprazole wakati wa kunyonyesha
Wakati wa kunyonyesha, mama asitumie aache kutumia omeprazole au mtoto aachishwe kunyonya kwa sababu dawa hii inaweza kusababisha madhara kwa mtoto. Uamuzi unategemea umuhimu wa dawa kwa mama kwa wakati huo.
Maudhi ya omeprazole
Maudhi madogo madogo ya Omeprazole
Maumivu ya kichwa(7%)
Maumivu ya tumbo(5%)
Kuharisha(4%)
Kichefuchefu(4%)
Kutapika(3%)
Kujamba(3%)
Kutopata choo(2%)
Kizunguzungu (2%)
Vipele kwenye ngozi(2%)
Kikohozi(1%)
Endapo umesahau dozi yako ya Omeprazole ufanyenini?
Dawa umesahau dozi ya omeprazole, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiri muda ufike kisha utumie dozi moja na kuendelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-