Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Mei 2020, 23:33:25
Pantoprazole
Ni dawa iliyo kundi la Protoni pumpu inhibita inayofanya kazi ya kuzuia uzalishaji wa tindikali tumboni.
Majina ya kibiashara
Pantoprazole hupatikana kwa jina jingine kama;
Protonix
Protium
Pantozol
Pantor
Pantoloc
Fomula ya kikemikali
Fomula ya kikemia ya Pantoprazole ni C16H15F2N3O4S
Jina la kisayansi (IUPAC)
Pantoprazole hufahamika kwa jina la kisayansi kama 6-(difluoromethoxy)-2-[(3,4-dimethoxypyridin-2-yl)methylsulfinyl]-1H-benzimidazole
Fomu na uzito wa Pantoprazole
Hupatikana kama vidonge vya
Miligramu 20
Miligramu 40
Dozi ya dawa ya kimiminika
Pakiti yenye miligramu 40
Dozi ya kuchoma kwa sindano;
Kila kichupa ina miligramu 40.
Pantoprazole hutibu nini?
Pantoprazole hutumika yenyewe au pamoja na dawa zingine katika matibabu ya;
Vidonda vya tumbo.
Vidonda vya tumbo vinavyo sababishwa na dawa zilizopo kwenye kundi la NSAID.
Sindromu ya Zollinger-Ellison.
Kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni baada ya upasuaji
Kutibu kucheua tindikali- Gastroesofajio rifluksi
Kutibu michubuko kwenye koo la chakula kutokana na tindikali.
Namna Pantoprazole inavyofanya kazi
Huzuia seli za gastrini katika tumbo kuzalisha tindikali
Ufyonzwaji wa Pantoprazole
Hufyonzwa hadi kwa asilimila 77 kama ukinywa
Huanza kuafanya kazi baada ya saa 24 baada ya kumezwa na kama imetolewa kupitia mshipa wa damu huanza kufanya kazi mara baada ya kutolewa.
Huweza kufanya kazi hadi kwa siku 7
Nusu maisha ya Pantoprazole
Nusu ya dawa hutumika mwilini baada ya saa 1.
Utoaji Pantoprazole mwilini
Pantoprazole na mabaki yake hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo (asilimia 71) na kwenye kinyesi (asilimia 18).
Maudhi ya Pantoprazole
Maudhi madogo ya Pantoprazole
Kichwa kuuma
Kuaharisha
Kichefuchefu
Maumivu ya tumbo
Kutapika
Kujamba
Kizunguzungu
Maumivu ya viungo
Homa kwa watoto.
Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji kwa watoto
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Pantoprazole
Marufuku kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii
Mgonjwa anaetumia dawa zenye rilpivirine
Angalizo la Pantoprazole
Kuhara wakati wakutumia dawa ya pantoprazole kunaweza kusababishwa na bakteria clostridium difficile.
Kutumia dawa hii kila siku zaidi ya mara moja kwa muda mrefu kunaongeza uwezekano wa mifupa kuvunjika kwa urahisi.
Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu kama zaidi ya miaka mitatu yaweza kusbabisha upungufu wa vitamini B-12 kwa kupunguza ufyonzwaji wa vitamini hizo.
Matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha kiwango cha magnesium kwenye damu kushuka chini ya kiwango cha kawaida.
Matumizi ya zaidi ya mwaka yanaongeza atari ya polipsi kwenye tezi zilizo kwenye fandazi.
Inaweza leta ugonjwa wa kusambaa wa lupazi erithromatosasi
Muingiliano wa Pantoprazole na dawa zingine
Ufyonzwaji wake hupungua ikitumika pamoja na sucralfate.
Pantoprazole hupunguza utendaji kazi wa dawa zifuatazo:-
Ketoconazole
Itraconazole
Digoxin
Dawa za chumvi zenye madini ya chuma
Erlotinib
Dasatinib
Kutumia kwa pamoja na dawa ya warfarin inaweza kusababisha kuvuja damu nyingi na kuhatarisha maisha. Inabidi kufuatilia muda wa prothrombini.
Huongeza kasi ya dawa ya theophylline kutolewa mwilini, hivyo ni muhimu kuongeza dozi ya theophylline ikiwa zitatolewa kwa pamoja.
Pantoprazole kwa mjamzito
Dawa itumike kwa tahadhari kama faida ya kutumia ni kubwa kuliko madhara; Majaribio kwa wanyama yanaonesha madhara na majaribio kwa binadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama na kwa binadamu hayajafanyika.
Pantoprazole wakati wa kunyonyesha
Ni vyema kujitahidi kuepuka matumizi ya dawa hii wakati wa kunyonyesha kwani hufika kwenye maziwa ya mama na inaweza kumdhuru mtoto anaye nyonya. Uamuzi wa kuitumia wakati wakati wa kunyonyesha utategemea faida na hasara za kuitumia.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-