top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

31 Machi 2020 13:59:31

Potasiamu

Potasiamu

Potasiamu ni moja ya madini muhimu mwilini, hufanya kazi nyingi ikiwa pamoja na kusafirisha umeme kwenye mishipa ya fahamu.


Madini haya hupatikana kwa wingi ndani ya seli kuliko nje. Ili seli, misuli na mishipa ya fahamu iweze kufanya kazi inahitaji madini haya ya potasiamu.


Mwili hudhibiti iwango cha madini kiwe kile kinachotakiwa ndani nan je ya seli,madini haya yakizidi husababisha dalili na tatizo la haipakalemia, na yakipungua husababisha dalili na tatizo la haipokalemia

Baadhi ya dalili zinazohusiana na kiwango kisicho sawia katika damu ni kama moyo kwenda ndivyo sivyo, uchovu wa misuli, uchovu mkali wa mwili, kichefuchefu, misuli kuuma na kubana, upumuaji wa shida, maumivu ya kifua kutokana na moyo, matatizo ya kumeng’enya chakula, ganzi na miguu kuwaka moto, na kubadilika kwa hali ya moyo.


Hata hivyo mwili huwez akutumia akiba yake ya potasiamu ili kuhakikisha kiwango kinakuwa sawia kwenye damu.


Baadhi ya vitu vinavyoweza kusababisha madini haya kutokuwa kwenye kiwango kinachotakiwa ni;

  • Kutapika

  • Magonjwa sugu ya figo

  • Matumizi makubwa ya dawa za kuharisha

  • Kutokwa na jasho sana

  • Matumizi makubwa ya pombe

  • Kuharisha

  • Diabetic ketoasidosisi

  • Matumizi ya dawa za duretiki

  • Upungufu wa madini ya foliki aside

  • Aldesteroinizimu ya awali

  • Baadhi ya matumizi ya dawa za antibayotiki



Endapo utashukiwa kuwa na kiwango kisicho kawaida cha madini ya potasiamu mwilini, daktari wako atakufanyia vipimo mbalimbali kisha kukupa tiba inayofaa.


Dawa zinazoongeza madini ya potasiamu mwilini


  • Aldactone. (spironolactone)

  • potassium chloride ER

  • Micro-K. potassium chloride ER

  • Epiklor.

  • Vyakula vyenye madini ya potasiamu kwa wingi mfano wake ni

  • Ndizi

  • Machungwa

  • Boga

  • Tunda la apikroti

  • Matunda ya kukaushwa kama tende na zabibu

  • Spinachi ya kupikwa

  • Brokoli iliyopikwa

  • Viazi

  • Uyoga

  • Kunde

  • Mimea jamii ya tango

  • Bilinganya

  • Mimea jamii ya mabogo

  • Mboga za kijani

  • Samaki aina kadhaa kama tuna,

  • Mbegu jamii ya kunde kama maharagwe na kunde

  • Korosho

  • Chumvi

  • Nyama

  • Wanyama jamii ya ndege

  • Mpunga wa brauni

  • Ngano

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:24:46

Rejea za mada hii:-

1.James L. Lewis, III. Overview of Potassium's Role in the Body. https://www.msdmanuals.com/home/hormonal-and-metabolic-disorders/electrolyte-balance/overview-of-potassium-s-role-in-the-body. Imechukuliwa 29.03.2020

2.MEDICALNEWSTODAY. What to know about high potassium.https://www.medicalnewstoday.com/articles/324913. Imechukuliwa 29.03.2020.

3.James L. Lewis, III , MD,Hypokalemia (Low Level of Potassium in the Blood). https://www.msdmanuals.com/home/hormonal-and-metabolic-disorders/electrolyte-balance/hypokalemia-low-level-of-potassium-in-the-blood. Imechukuliwa 29.03.2020

4.Hypokalemia. The Merck Manuals: The Merck Manual for Health Care Professionals. http://www.merckmanuals.com/professional/endocrine_and_metabolic_disorders/electrolyte_disorders/hypokalemia.html. Imechukuliwa 29.03.2020

5.Mount DB, et al. Clinical manifestations and treatment of hypokalemia in adults. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 29.03.2020

6.Hypokalemia medication. https://www.goodrx.com/hypokalemia/drugs. Imechukuliwa 29.03.2020.

7.Maswali na majibu kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC
bottom of page