Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
31 Mei 2020, 15:52:02
Ramipril
Utangulizi
Ramipril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Altace.
Ramipril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa;
• 1.25mg
• 2.5mg
• 5mg na
• 10mg
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu;
Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na ramipril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu.
Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin.
Kutanuka kwa mishipa ya damu husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
• Benazepril (Lotensin, Lotensin Hct)
• Captopril (Capoten)
• Enalaprili (Vasotec)
• Fosinopril (monopril)
• Lisinopril (Zestril, Prinivil, Qbrelis)
• Moexipril (Univasc)
• Perindopril (Aceon)
Kazi za dawa ni kama ifuatavyo;
• Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
• Hutumika kwa kuzuia riski ya kiarusi na mayocardio infaksheni
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
• Aliskiren
• Sacubitril/valsartan
• Aspirin
• Azilsartan
• Candesartan
• Celecoxib
• Diclofenac
• Diflunisal
• Eprosartan
• Etodolac
• Fenoprofen
• Flurbiprofen
• Ibuprofen
• Indomethacin
• Irbesartan
• ketoprofen
• Ketorolac
• Lofexidine
• Losartan
• Meclofenamate
• Mefenamic acid
• Meloxicam
• Nabumetone
• Naproxen
• Olmesartan
• Oxaprozin
• Piroxicam
• Pregabalin
• Sacubitril/valsartan
• Salsalate
• Sulindac
• Telmisartan
• Tolmetin
• Valsartan
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya ACEIs
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
• Wagonjwa walioferi ini
• Wagonjwa wenye shinikizo la chini la damu
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi ni;
• Dawa nusu ya maisha yake kwenye mwili ni kati ya masaaa 2 mpaka 4
• Dawa hii hutolewa asilimia 60 kwa njia ya mkojo na asilimia 40 kwa njia ya kinyesi
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi D la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito
Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni. Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila hapendekezwi kutumika kwa mama anayenyonyesha.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
• Maumivu ya kichwa
• Kukohoa
• Kizunguzungu
• Kichefuchefu
• Kuharisha
• Shikizo la chini la damu
• Kutapika
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:37
Rejea za mada hii:-