Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Mei 2020, 08:37:00

Rosiglitazone
Rosiglitazone ni dawa mojawapo ya kutibu kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la thiazolidinedione.
Majina ya kibiashara ya Rosiglitazone
Rosiglitazone huwa maarufu kwa jina Avandia.
Matumizi ya Rosiglitazone na chakula
Rosiglitazone inaweza kumezwa pamoja au bila chakula mara moja au mbili kwa siku kama utakavyoelekezwa na Daktari.
Fomu na uzito wa Rosiglitazone
Rosiglitazone hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;
2mg
4mg
Nusu maisha ya Rosiglitazone
Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 3 hadi 5 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 3 hadi 4.
Utoaji dawa Rosiglitazone mwilini
Mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 64 na Kinyesi asilimia 22.
Namna Rosiglitazone dawa inavyofanya kazi
Dawa jamii ya thiazolidinedione ikiwemo Rosiglitazone hufanya kazi zifuatazo ili kuthibiti kiasi cha sukari mwilini;
Huchochea risepta za Peroxisome Proliferator zilizo kwenye tezi ya kongosho ili zishinikize uzalishaji wa homon insulin kwa ajili ya kufanya kazi ya kuongeza matumizi ya sukari mwilini na kubadilisha kiwango kingine kuwa glukagoni kisha kuhifadhi mwilini. Kwa kuongeza uzalishaji wa insulin, dawa hii husababisha kushusha kiwango cha sukari wkenye damu.
Dawa kundi moja na Rosiglitazone
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la thiazolidinedione) na dawa hii ni;
Pioglitazone
Troglitazone
Rosiglitazone hutibu nini?
Hutumika kushusha sukari kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa kisukari aina ya II
Upekee wa Rosiglitazone
Haisababishi sumu kwenye ini tofauti na dawa zingine kwenye kundi moja.
Mwingiliano wa Rosiglitazone na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Eluxadoline
Ethanol
Gemfibrozil
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Rosiglitazone
Rosiglitazone haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine jamii ya thiazolidinedione.
Wagonjwa wenye moyo ulioferi.
Angalizo
Rosiglitazone inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wa kisukari aina ya I
Huweza kupelekea kuongezeka kwa uzito inapotumika pamoja na dawa zingine za kumeza za kisukari.
Huweza kupelekea yai kutolewa kwa wanawake walio hatua za awali za komahedhi
Matumizi ya Rosiglitazone kwa mama mjamzito
Tafiti zilizofanyika kwa wanyama zinaonyesha hakuna madhara katika ukuaji wa mtoto ilipotolewa kwa panya na sungura wenye mimba hivyo inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni kubwa kuliko hatari kwa mama au mtoto.
Matumizi ya Rosiglitazone kwa anayenyonyesha
Hakuna taarifa juu ya upatikanaji wa dawa hii kwenye maziwa hivyo inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida ni nyingi kuliko hatari kwa mtoto.
Maudhi ya Rosiglitazone
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kuongezeka kwa kiwango cha kolestro mwilini
Kuongezeka kwa Sshinikizo la damu
Moyo kuferi
Kuharisha
Maambukizi ya juu ya mfumo wa upumuaji
Kichwa kuuma
Kuongezeka uzito
Sukari kushuka
Maumivu ya misuli
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako ya rosiglitazone tumia mara pale utakapokumbuka. Eendapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiri ufike kisha utumie kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-