Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Aprili 2020, 08:49:13

Semaglutide
Semaglutide ni dawa mojawapo ya kutibu kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la Glucagon like peptide 1 Agonisti.
Majina ya kibiashara ya Semaglutide
Dawa hii huwa maarafu kwa majina ya Ozempic na Rybelsus na hupatikana katika mfumo wa kidonge na majimaji.
Fomu na uzito wa Semaglutide
Dawa (Ozempic) hupatikana katika mfumo wa maji kwa ajili ya sindano katika uzito wa 1.34mg/mL
Pia hupatikana katika mfumo wa kidonge (Rybelsus) chenye uzito wa Milligramu zifuatazo;
3mg
7mg
14mg
Namna Semaglutide inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuchochea kongosho kuzalisha homoni ya Insulin mara kiwango cha sukari kinapoongezeka kwenye damu.
Homoni ya Insulini husaidia seli za mwili kutumia na kuhifadhi sukari na hivyo kuiondoa kwenye dmau. Kufanya hivi kiwango cha sukari hupungua sana kwenye damu.
Dawa kundi moja na Semaglutide
Dawa kundi moja na Semaglutide (Glucagon Like Peptide 1 Agonisti) ni;
Liraglutide
Taspoglutide
Lixisenatide
Dulaglutide
Semaglutide hutibu nini?
Hutumika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa Wagonjwa wenye kisukari aina ya pili, pia hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (GlP1 Inhibita):
Humfaa mgonjwa wa kisukari ambaye Metformin imeshindwa kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
Sio gharama kwa matumizi kwa mgonjwa wa kisukari sababu hutumika mara moja kila siku kwa siku 7 ukilinganisha na dawa zingine kwenye hili kundi.
Mwingiliano wa Semaglutide na dawa zingine
Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;
Tolbutamide
Tolazamide
Repaglinide
Nateglinide
Insulin lispro
Insulin isophane human
Insulin inhaled
Insulin glulisine
Insulin glargine
Insulin detemir
Insulin degludec
Insulin aspart
Ifosfamide
Glyburide
Glipizide
Glimepiride
Chlorpropamide
Wagonjwa wasioapswa kutumia Semaglutide
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hiyo
Mwenye shida ya figo
Angalizo
Sio mbadala wa Insulin
Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari aina ya kwanza
Huweza kupelekea kuvimba kwa kongosho
Huweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi
Huweza kupelekea uvimbe kwenye seli C za tezi ya thairoidi
Wagonjwa wanaotibiwa na dawa hii wameripotiwa kupata dayabetiki retinopathi
Matumizi ya Semaglutide kwa mama mjamzito
Kutokana na tafiti zilizofanywa kwenye uzazi wa wanyama, zipo hatari kwa mtoto. Endapo Semaglutide itatumika kwa mama mjamzito inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida ni nyingi zaidi ya hatari kwa mtoto
Matumizi ya Semaglutide kwa mama anayenyoneysha
Kwa mama anayenyonyesha hakuna taarifa kamili, tafiti zinaonyesha Semaglutide kuingia maziwa ya panya anayenyonyesha. Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha endapo faida zitakuwa nyingi zaidi ya hatari kwa mtoto
Maudhi ya Semaglutide
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kichefuchefu
Sukari kushuka
Kichefuchefu
Maumivu ya tumbo
Kuharisha
Choo kuwa kigumu
Tumbo kujaa gesi
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Kama ukisahau dozi yako ya Semaglutide, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiri ufike kisha tumia kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:24:06
Rejea za mada hii:-