Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Machi 2020 13:44:01
Sulfamethoxazole na Trimethopin
Sulfamethoxazole na Trimethopin ni dawa ya antibayotiki ambayo imepewa ufupisho wa Co – Trimoxazole inayotumika katika matibabu ya maradhimbalimbali yanayosababishwa na bakteria.
Bakteria wanaodhuriwa na Co – Trimoxazole
Baadhi ya bakteria ambao hutibiwa na dawa hii ni bakteria jamii ya:
Staphylococcus aureus
Staphylococcus epidermidis
Staphylococcus pyogenes
Streptococci kundi la Viridans
Escherichia coli
Proteus mirabilis
Proteus morganii
Proteus rettgeri
Salmonella typhi
Klebsiella species
Brucella abortus
Yersinia enterocolitica
Co – Trimoxazole hutibu nini?
Dawa ya jamii ya Sulfamethoxazole na Trimetropin hutumika kutibu magonjwa yafuatayo:
UTI
Bronkaitizi
Shigellosisi (Ugonjwa wa kuhara ambao huambatana na tumbo kuuma)
Kuhara kwa muda mfupi -kunaosababishwa na bakteria wa Escherichia Coli
Nimonia ya Pneumosisti jirovesii: Nimonia ambayo hutokea sana kwa wagonjwa wa VVU na UKIMWI
Homa ya mapafu ya kuambukizwa kwenye jamii
Maisetoma
Otaitizi media
Maudhi ya Co – Trimoxazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na:
Kukosa hamu ya kula
Kichefuchefu
Kutapika
Kutokwa na Vipele
Anemia ya Aplastiki
Kupata mzio
Kuwashwa ngozi
Haipakalemia
Upungufu wa Foleti mwilini
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Co – Trimoxazole
Dawa hii haitumiki kwa watu wafuatao :
Watoto chini ya miezi miwili
Mama mjamzito anayekaribia kujifungua (Term pregnancy)
Kwa mtu mwenye anemia ya meganoblastic
Watu wenye matatizo ya ini
Watu wenye matatizo ya figo
Matumizi ya Co – Trimoxazole kwa mama mjamzito
Kwa maelezo kuhusu mama mjamzito ingia kwenye sehemu ya ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha ndani ya tovuti hii.
Matumizi ya Co – Trimoxazole wakati wa kunyonyesha
Kwa maelezo kuhusu mama mjamzito ingia kwenye sehemu ya ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha ndani ya tovuti hii.
Kama umesahau dozi ya Co – Trimoxazole ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Co – Trimoxazole , tumia pale utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana. Endapo muda wa dozi nyingine umekaribia saba achana na dozi uliyosahau kisha subiria muda ufike na endelea na dozi kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:22:37
Rejea za mada hii:-