Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Aprili 2020, 09:39:47
Truvada
Dawa hii ni muunganiko wa dawa mbili ambazo ni Tenofovir na Emtricitabine (FTC). Truvada ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI (ART) na ni muunganiko wa dawa mbili zilizo kwenye makundi ya NRTIs na NtRTIs
Truvada itumike na chakula?
Truvada inaweza kutumika pamoja au pasipo chakula.
Truvada hutibu nini?
Dawa hii huwa na kazi ya
Kupunguza hatari ya kupata UKIMWI kwa watu waliokwisha jihatarisha. Mifano ya makundi haya ni watu wanaojiuza miili kwa ngono, mashoga, wanaojiduga madawa ya kulevya n.k. kumbuka mgonjwa anatakiwa kuwa hana VVU ili kutumia Truvada. Pia dawa hii haitibu/haizuii kupata maambukizi ya zinaa wala ujauzito
Kutibu mgonjwa mwenye homa ya Ini na HIV-1 kwa pamoja
Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyo atakavyoelekezwa na daktari
Dawa zisizopaswa kutumika na Truvada
Truvada haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Abacavir
Acyclovir
Diclofenac
Efavirenz
Zidovudine
Nevirapine
Ibuprofen
Ganciclovir
Ribavirin
Lamivudine
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Truvada
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wenye mzio na dawa hii
Ambao bado hawajui hali yao ya maambukizi ya VVU au kwa mtu mwenye UKIMWI
Angalizo
Inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wagonjwa wafuatao:
Ini zilizovimba sana
Haipaswi kuchanganywa na dawa zingine zenye Emtricitabine au Tenofovir
Matumizi ya Truvada kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonyesha kuwa Truvada haina madhara kwa mtoto wakati wa ujauzito
Matumizi ya Truvada kwa mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonyesha kuwa Truvada hupita na kuingia kwenye maziwa lakini haina madhara kwa mtoto.
Maudhi ya Truvada
Baadhi ya maudhi madogo ya Truvada ni pamoja na:
Kuchoka
Kichwa kuuma
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kizunguzungu
Misuli kukosa nguvu
Ndoto zisizo za kawaida
Tumbo kuuma
Kukosa usingizi
Kizunguzungu
Endapo umesahau dozi yako ya Truvada ufanyaje?
Dawa hii hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti HIV endapo utasahau dozi yako, tumia muda uliokumbuka na Kuendelea na muda huo siku inayofuata kama ulivyoelekezwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 17:02:22
Rejea za mada hii:-