Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Aprili 2020 20:45:10
Acarbose
Acarbose ni dawa inayotumika kushusha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii hutumika kuzuia ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu mara baada ya kula. Acarbose hutumika pamoja na mazoezi na lishe sahihi kwa wagonjwa wa kisukari ili kudhibiti ongezeko la sukari kwenye damu.
Upekee wa dawa
Haisababishi kushuka kwa kiwango cha sukari kupita kiasi kama itatumika yenyewe.
Majina ya kibiashara ya dawa
Precose
Miglitol(Glyset)
Voglibose
Glucobay
Glucor
Glumida
Prandase
Fomula ya kikemikali
C25H43NO18
Muonekano
Ni dawa ya kidonge. Umbo na rangi vinaweza kutofautiana kutegemeana na kiwanda kinachozaliza.
Dozi zinazopatikana
Hupatikana kwa vidonge vya:-
Miligramu 25
Miligramu 50
Miligramu 100
Namna ya kutumia
Meza kama utakavyo elekezwa na daktari wako.
Unashauriwa kumeza dakika 30 kabla ya kula chakula.
Namna inavyofanya kazi mwilini
Dawa hii huchelewesha kumeng'enywa kwa vyakula wanga ili kuzuia kutengenezwa kwa sukari na hivyo kuzuia ongezeko la sukari kwenye damu mara baada ya kula.
Umetaboli wa dawa
Dawa hii huchakatwa na mwili ndani ya utumbo mdogo wa chakula.
Huanza kufanya kazi baada ya saa 1.
Taka mwili ya mabaki ya dawa ya acarbose hutolewa kwenye kinyesi (asilimia 51) na mkojo(asilimia 34).
Wagonjwa wasiopasswa kutumia
Wagonjwa walioferi figo
Wagonjwa wenye mzio na dawa ya acarbose
Wagonjwa waliowahi kupata dayabetiki ketoasidosisi
Wagonjwa waliopata tatizo la kuziba utumbo
Wagonjwa wenye vidonda vya tumbo
Wagonjwa wenye figo iliyoferi
Tahadhari wakati wa kutumia acarbose
Bado hakuna tafiti za kutosha kuelezea uhusiano wa dawa ya acarbose na hatari zake katika mfumo wa moyo na mishipa ya damu.
Kama ikitumiwa na insulin au sulfonylurea inaweza kushusha sukari kupita kiasi.
Inaweza kushindwa kufanya kazi vizuri kwa wagonjwa wenye maambbukizi au homa, upasuaji mkubwa au majeraha makubwa.
Matumizi wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Inaweza kutumiwa kwa mama mjamzito ila hakuna tafiti za kutosha kuhusu mdahara yake. Epuka kwa kipindi cha kunyonyesha. Ni vema kufuata ushauri wa daktari wako.
Maudhi ya dawa
Tumbo kujaa gesi
Kujamba
Kuharisha
Kuwashwa ngozi
Huweza kusababisha kuferi kwa ini
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:50:44
Rejea za mada hii:-