top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

23 Aprili 2020, 08:07:55

Acetohexamide

Acetohexamide

Acetohexamide ni dawa kwenye kundi la sulphonylurea inayotumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili.


Majina ya kibiashara


  • Dimelin

  • Dymelor

  • Gamadiabet


Fomula ya kikemikali


C15H20N2O4S


Jina la kitiba


3-(4-acetylbenzenesulfonyl)-1-cyclohexylurea.


Muonekano wa acetohexamide ni upi?


Kidone cheupe, haina harufu.


Dozi inayopatikana


Hupatikana kama kidonge cha miligramu 500


Sababu za kutumia


Ugonjwa sukari ya juu isiyo tibika kwa insulini ikiwa mlo na mazoezi havitoshi kurekebisha kiwango cha sukari.


Inafanyaje kazi mwilini?


Inashusha kiwango cha sukari kwenye damu kwa:-


  • Kuchochea seli za kongosho kuazalisha homoni ya insulini.

  • Inasaidia mwili kuweza kutumia insulini inayozalishwa.

  • Insulin inayozalishwa hufanya kazi


Huingia kwenye damu kwa njia gani?


Acetahexamide humezwa kwakua hufyonzwa upesi kutoka kwenye mfumo wa chakula kuingia kwenye damu.


Umetaboli wa dawa kwenye ini


Acetohexamide huvunjiwa kwenye ini na kutoa kemikali hydroxyhexamide ambayo ndiyo haswa hufanya kazi ya kushusha sukari.


Utoaji wa taka za dawa


Takamwili za mabaki ya acetohexamide hutolewa kwa njia ya mkojo.


Muda wa ufanyaji kazi


Kiwango kwenye damu hufikia kilele baada ya saa 3. Hufanya kazi mwilini kwa saa 12-24.


Hufaa zaidi kwa wagonjwa wapi?


  • Wenye mzio na dawa ya insulin

  • Wagonjwa wa gauti (Ndiyo sulfonylurea pekee inayo ongeza kasi ya mwili kutoa tindkali kutokana urea (yuriki asidi) hivyo kupunguza athari za gauti.

  • Wenye Uono hafifu

  • Wagojwa walio katika hatari ya sukari kushuka zaidi mwilini kwa kutumia dawa ya insulin


Tahadhari


Isitumike kwa mgonjwa mwenye


Matatizo kwanye mfumo wa damu mfano saratani ya damu na upungufu wa damu.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia


  • Kisukari aina ya kwanza

  • Kisukari cha ujauzito

  • Ini linaloshindwa kufanya kazi

  • Figo inayoshindwa kufanya kazi

  • Wagonjwa wa sukari waliopata shida ya maambukizi makali, upasuaji mkubwa, au asidosisi


Muingiliano na dawa nyingine


Dawa zifuatazo zinaongeza atari ya kushuka kwa sukari zikituiwa na acetohexamide;

  • Sulfonamides,

  • Propranolol

  • Salicylates

  • Phenylbutazone

  • Probenecid

  • Dicumarol

  • Chloramphenicol

  • Monoamine oxidase inhibita

  • Kutumia pamoja na captopril na enalapril ambazo hutibu shikizo la juu la damu hakuna madhara.


Matumizi wakati wa kunyonyesha


Inaweza kushusha sukari ya mtoto anaenyonya na hivyo ni hatari kwa mtoto. Hivyo daktari anaweza kuibadili. Fuatilia kama mtoto anaenyonya ataonesha dalili za sukari kushuka kama vile kuchoka, kushindwa kunyonya,kushindwa kula, degedege, joto la mwili kushuka, kiwango cha sukari kwenye damu ya mtoto.


Epuka


Kutumia na pombe


Maudhi madogo madogo


  • Kichefuchefu

  • Kutapika kuharisha

  • Maumivu ya kichwa

  • Tumbo kujaa

  • Kiungulia

  • Athari kwenye ngozi kama vipele, kuwashwa

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:51:07

Rejea za mada hii:-

1.Pubchem:https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Acetohexamide imechukuliwa 22/04/2020.

2.WebMD: https://www.webmd.com/drugs/2/drug-14352/acetohexamide-oral/details imechukuliwa 22/04/2020.

3.Drugbank: https://www.drugbank.ca/drugs/DB00414 imechukuliwa 22/04/2020.

4.RXwiki. https://www.rxwiki.com/acetohexamide. Imechukuliwa 22.03.2020

5. Drugs during pregnancy and lactation by christof chaefer etal. Toleo la pili 2007, ISBN: 978-0-444-52072-2
bottom of page