Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
2 Mei 2020, 19:43:25
Azilsartan
Azilsartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini II Risepta bloka. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Edarbi.
Rangi ya dawa
Rangi ya dawa hii ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.
Azilsartan inapaswa kutumika pamoja na chakula au pasipo chakula mara moja kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari wako.
Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Dozi utakayopewa itategemea hali yako ya kiafya na jinsi mwili unavyokubali matibabu
Kukusaidia kukumbuka dozi yako, tumia muda sawa wa kunywa dawa kila siku. Ni muhimu kuendelea kutumia dawa hii hata kama haujisikii kuumwa maana mara nyingi wagonjwa wa shinikizo la juu la damu huwa hawaonyeshi dalili za kuumwa.
Uzito wa dawa
Azilsartan hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;
40mg
80mg
Namna dawa inavyofanya kazi ili kupunguza shinikizo la damu;
Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Azilsartan hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;
Hufanya kazi kwa kufunga risepta za Angiotensin II zinazojulikana kwa jina la AT1 Risepta. Risepta hizi hupatikana kwenye moyo,mishipa ya damu na figo. Risepta hizi zinapofungwa hupelekea kutanuka kwa mishipa ya damu hivyo kuwa na kipenyo kikubwa na matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.
Hupinga uzalishwaji wa homoni ya Aldosterone ambayo hutumika kuthibiti kiasi cha sodium na maji. Kiasi cha sodiamu kinapothibitiwa huweza kupunguza shinikizo la damu kwa hutanua kipenyo cha mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo la juu
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na ARBs ni;
Candesartan
Olmesartan
Eprosartan
Irbesartan
Losartan
Telmisartan
Kazi ya dawa
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu pamoja na dawa zingine za kushusha shinikizo la damu kama Diuretics
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (ARBs) ni;
Huwa na uwezo mkubwa wa kupunguza shinikizo la juu la damu la Systollic kwa masaa 24 ya kwanza kupita dawa zingine za kwenye kundi hili
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Benazepril
Captopril
Enalapril
Fosinopril
Lisinopril
Lithium
Lofexidine
Moexipril
Perindopril
Potassium Phosphate IV
Quinapril
Ramipril
Trandolapril
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za ARBs pia haipaswi kutumika pamoja na dawa ya Aliskiren kwa wagonjwa wa kisukari
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye Haipakalemia
Wagonjwa wenye Haipotension
Wagonjwa wenye shida ya figo
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Kwa mama mjamzito haipaswi kutumika, itumike tu endapo endapo faida za dawa ni kubwa kuliko madhara kwa mtoto. Madhara kwa mtoto ni haipotension, figo kuferi na kifo.
Mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama inatolewa kwenye maziwa
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kichefuchefu
Kuharisha
Misuli kukaza
Kizunguzungu
Haipotension
Angioedema
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:49:58
Rejea za mada hii:-