Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
7 Aprili 2020, 18:55:22
Clindamycin
Ni antibiotiki iliyo kwenye kundi la lincosamide inayotumika kutibu maambukizi makali ya bakteria wanaouliwa na dawa hii pamoja na kutibu chunusi za vulgarizi. Kemikali ya lincosamide huvunwa kutoka kwa bakteria anayeitwa Streptomyces lincolnensis.
Clindamycin hutibu bakteria aina ya anaerobiki pamoja na gram- chanya cocci na bacilli and gram-hasi bacilli. Kwa kushangaza dawa hii pia inaonekana kuua baadhi ya protozoa na imekuwa ikitumika mbali na matumizi yake iliyoelekewa, ili kutibu toksoplasmosis, maleria na babesiosisi.
Clindamycin huvunjwa na Ini kabla ya kutolewa mwilini, Figo na mfumo wachakula huhusika kusafisha dawa hii kwa kuitoa nje ya mwili.
Fomu na uzito wa dawa ya Clindamycin
Dawa ya clindamycin hupatikana kwenye mfumo wa tembe, majimaji ya kuchoma sindano au ya kuwekewa kwenye mishipa ya damu. Dawa hii huwa na uzito wa
150-300mg kwa Kidonge
2ml ( 150mg/ml) kwa dawa ya Sindano
10g kwa krimu au jeli
Bakteria wanaouliwa na Clindamycin
Baadhi ya bakteria ambaowanauliwa na Dawa hii huwa Ni bacteria jamii ya
Staphylococci
Streptococci
Pneumococci
Magonjwa yanayotibiwa na Clindamycin
Dawa Clindamycin hutibu magonjwa yafuatayo
Kutibu magonjwa ya ngozi na tishu laini
Kutibu magonjwa ya mfumo wa upumuaji njia ya juu mfano neumonia
Kutibu maambukizi katika mfumo wa uzazi kwa wanawake
Kutibu mifupa na maungio
Kutibu maambukizi ya uti wa mgongo
Kutibu magonjwa ya kuambukiza yaliosababishwa na vimelea ( septicaemia)
Maudhi ya matumizi ya Clindamycin
Baadhi ya maudhi madogo madogo ya Dawa Ni pamoja na;
Kuharisha
Kutapika
Kuwashwa ngozi
Kupata Upele( rashes)
Homa
Maumivu ya tumbo
Mwili kuwa na uchovu
Maumivu ya kichwa
Misuli kuuma
Kukosa hamu ya chakula
Kupata manjano katika macho, ngozi
Kushindwa kupumua vizuri
Maumivu ya kifua
Kuhisi kizunguzungu
Ngozi kuvimba na kupata uwekundu
Dawa zisizopaswa kutumika na Clindamycin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kwa sababu madhara makubwa yanaweza kutokea zikitumika kwa pamoja;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo ya kipindupindu
Erythromycin
Chanjo hai ya Typhoid
Cisatracurium
Onabotulinumtoxina
Pancuronium
Rapacuronium
Rimabotulinumtoxinb
Rocuronium
Succinylcholine
Vecuronium
Atracurium
Angalizo kwa watumiaji wa Clindamycin
Tumia Dawa hii kwa Umakini kwa wagonjwa hawa;
Wenye shida ya Ini
Wenye shida ya Figo
Kwa mama wajawazito na wanao nyonyesha
Wazee
Wenye historia ya kua na pumu(asthma)
Wenye matatizo ya mzio kwenye ngozi( kama pumu ya ngozi- eczema)
Matumizi ya Clindamycin wakati wa ujauzito
Dawa hii itumiwewakati wa ujauzito endapo faida zinazidi hasara.
Matumizi ya Clindamycin Wakati wa kunyonyesha
Dawa hii hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama, dawa kwa mtoto anayenyonya huwa na madhara kiasi kama kuharisha, maambukizi ya kandida na mara chache damu kwneye kinyesi, damu kwenye kinyesi huwa ni dalili ya kolaitizi inayosababishwa na hii dawa.
Endapo umesahau dozi Clindamycin ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi kwenye muda uliopangiwa, tumia dawa hiyo mara utakapokumbuka. Ruka dozi uliyosahau endapo muda wa kutumia dozi nyinginr umekaribia sana.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:49:08
Rejea za mada hii:-