Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Juni 2020 19:23:47
Clonidine
Clonidine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha II Agonisti . Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Catapres na Catapres-TT
Rangi ya dawa
Rangi ya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza
Clonidine inapaswa kutumiwa pasipo au pamoja na chakula mara mbili kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari
Hakikisha unakunywa dawa kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa
Fomu na uzito wa dawa
Clonidine hupatikana katika mfumo wa kidonge na sindano chenye uzito wa milligramu zifuatazo:
Kidonge
0.1 mg
0.2 mg
0.3 mg
Kimiminika cha kuchoma
100 mcg/ml
500 mcg/ml
Namna dawa inavyofanya kazi;
Huchochea seli kwenye ubongo zenye jina la Alpha adrenorisepta na kupunguza shughuli za sympathetic kwenye mfumo wa kati wa neva na kupelekea mapigo ya moyo kwenda sawa na kupunguza shinikizo la juu la damu kwa kutanua kipenyo cha mishipa ya damu
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Alpha 2 Agonisti) na dawa hii ni;
Methyldopa
Tizanidine
Guanfacine
Lofexidine
Kazi ya dawa
Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Alpha 2 Agonisti)
Dawa hii hutumika kwa dozi ndogo kwa ajili ya kushusha shinikizo la juu la damu tofauti na dawa zingine kwenye kundi hili
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Perampanel
Pentazocine
Orphenadrine
Nebivolol
Nalbuphine
Nadolol
Morphine
Mirtazapine
Methadone
Meperidine
Maprotiline
Macimorelin
Lofexidine
Lofepramine
Levobunolol
Imipramine
Hydromorphone
Hydrocodone
Ethanol
Esmolol
Doxepin
Diltiazem
Desipramine
Codeine
Clomipramine
Butorphanol
Buprenorphine
Brigatinib
Bremelanotide
Bisoprolol
Betaxolol
Azelastine
Atenolol
Amoxapine
Amitriptyline
Alfentanil
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine jamii ya Alpha II Agonisti
Wagonjwa wenye historia ya maambukizi kwenye sehemu walizochomwa sindano.
Tahadhari ya dawa hii
Dawa hii ina hatari ya kupelekea haipotension pia huweza kupelekea midomo kukauka pamoja na shida kwenye figo.
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Kwa mama mjamzito
Hakuna dalili za hatari zilizojitokeza baada ya matumizi ya dawa hii hivyo inaweza kutumika kwa mama mjamzito
Kwa mama anayenyonyesha
Haina madhara yeyote yaliyoripotiwa kwa mama anayenyonyesha hivyo inaweza kutumika
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Mdomo kuwa mkavu
Maumivu ya kichwa
Kuchoka
Kizunguzungu
Haipotension
Woga na wasiwasi
Mengine yanayofanyika Mwilini
Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 3 hadi masaa 5 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 12 hadi masaa 16. Dawa hii hutolewa mwilini kwa asilimia 60 kwa njia ya mkojo
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-