top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

5 Juni 2022, 10:41:36

Dawa bisacodyl

Dawa bisacodyl

Bisacodyl Dawa


Bisacodyl ni dawa kwenye kundi la dawa za kulegeza matumbo na kuongeza utoaji haja kubwa. Hutumika katika matibabu haja kubwa kwa shinda, haja ngumu na kusafisha utumbo mpana kwa muda


Majina mengine ya bisacodyl


Bisacodyl hufahamika kwa majina ya kibiashara kama:


  • Dulcolax

  • Correctol

  • BisacEvac

  • Bisacolax

  • Codulax

  • Alophen

  • Feen A Mint

  • Fleet Stimulant Laxative

  • Laxit

  • Modane


Uzito na fomu ya bisacodyl


Bisacodyl hupatikana kama kidonge chenye uzito wa miligramu 5.


Dawa kundi moja na Bisacodyl


Dawa zingine zilizo kundi moja na bisacodyl ni zile ambazo huwa kundi la vilegeza matumbo na viongeza utoaji wa haja ngumu kama vile:


  • Sodium Docusate

  • Co-danthrusate

  • Glycerol

  • Senna

  • Sodium picosulphate

  • Oxyphenisatin


Bisacodyl hutibu nini?:


Bisacodyl hutumika kutibu kwa muda hali magonjwa yafuatayo:


  • Kinyesi kigumu

  • Kinyesi kutoka kwa shida (konstipesheni)

  • Kusafisha utumbo mpana kabla ya kufanyiwa uchuguzi


Namna bisacodyl inavyofanya kazi


Bisacodyl hufanya kazi kwa kuibughudhi misuli laini ya mfumo wa chakula na hivyo kuongeza peristalisis na haswa kupitia madhara yake ya kuamsha mishipa ya fahamu ya parasimpathetiki. Pia huongeza kiasi cha maji ndani ya utumbo kwa kuingilia uwezo wa matumbo kuweka uwiano wa maji na madini.


Wasiopaswa kutumia bisacodyl


Bisacodyl haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye hali, dalili na magonjwa yafuatayo:


  • Historia ya mzio wa dawa hii

  • Kuziba kwa matumbo

  • Hali kali ya kuziba kwa utumbo kutokana na kinyesi

  • Dalili za maambukizi kwenye kidole tumbo

  • Kutapika

  • Kutokwa damu kwenye puru


Tahadhari za kuchukuliwa kwa watumiaji wa bisacodyl


  • Usitumie kwa muda mrefu inaweza kusababisha mwili wako ukawa tegemezi kwenye dawa

  • Kama una harisha na kutapika, usitumie dawa hii

  • Usitafune kidonge, meza kwa maji

  • Usitumie saa 1 baada ya kunywa dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali

  • Haipaswi kutumika kwa watoto chini ya miaka 6

  • Haipaswi kutumika zaidi ya wiki 1

  • Baadhi ya fomu ya dawa hutiwa benzyl alcohol ambayo imeonekana kuambatana na usumu kwa vichanga. Usitumie dawa yenye kemikali hii au mazao yake kwa vichanga.


Matumizi ya bisacodyl na pombe


Unaweza kutumia bisacodyl na pombe, hata hivyo usitumie pombe nyingi pamoja na dawa hii.


Ufyonzwaji wa bisacodyl


Asilimia 16 tu ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye damu


Muda kuanza kazi - bisacodyl


Mara baada ya kutumia bisacodyl, huanza kufanya kazi baada ya masaa 6 hadi 10.


Nusu maisha ya bisacodyl


Bisacodyl huwa na nusu maisha ya masaa 8


Utoaji wa bisacodyl mwilini


Bisacodyl kwa kiasi kikubwa hutolewa mwilini upitia haja kubwa


Matumizi ya bisacodyl kwa mama mjamzito


Kiasi kidogo cha dawa huingia kwenye damu, matumizi ya muda mfupi yanachukuliwa kuwa salama. Epuka matumizi ya muda mrefu ya bisacodyl wakati huu.


Matumizi ya bisacodyl kwa mama anayenyonyesha


Hakuna kiwango cha dawa kilichogunduliwa kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha. Kama itatumika wakati huu, inapaswa kutumika kwa tahadhari.


Dawa zenye mwingiliano mkali na bisacodyl


Dawa zifuatazo huwa na mwingiliano mkali hivyo hazipaswi kutumika pamoja na bisacodyl:


  • Sodium sulfate/magnesium sulfate/potassium chloride

  • Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate

  • Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate/polyethylene glycol


Dawa zenye mwingiliano wa wastani na bisacodyl


Dawa zifuatazo huwa na mwingiliano wa wastani na bisacodyl, kama zitatumika pamoja, mgonjwa anapaswa kuwa chini ya uchunguzi wa karibu wa mtaalamu wa afya:


  • Deflazacort

  • Dichlorphenamide

  • Potassium citrate


Dawa zenye mwingiliano mdogo na bisacodyl


Dawa zifuatazo huwa na mwingiliano mdogo na bisacodyl


  • Potassium acid phosphate

  • Potassium chloride


Maudhi ya bisacodyl


Baadhi ya maudhi ya bisacodyl ni:


  • Kunyonga kwa tumbo

  • Kupotea kwa uwiano wa madini na maji mwilini

  • Kuhara sana

  • Kichefuchefu

  • Hisia za kuungua kwenye puru

  • Kuona vitu vinazunguka

  • Kutapika


Je endapo umesahau kutumia dozi ya bisacody ufanyaje ?


Kama umesahau kutumia dozi ya bisacodyl, tumia mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa kunywa dozi nyingine umefika ambapo utapaswa kusubiria muda ufike ndipo utumie dozi hiyo na kuendelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.


Uhifadhi ya bisacodyl


Hifadhi dawa yako katika joto la mzingira (nyuzi joto za sentigrade 20 hadi 30). Usiweke kwenye friji au sehemu yenye mwanga wa jua au joto ili kuepuka kuharibu dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

20 Septemba 2023, 18:36:19

Rejea za mada hii:-

1. Examples of stimulant laxatives. https://gpnotebook.com/en-au/simplepage.cfm?ID=2114322506. Imechukuliwa 05.06.2022

2. Bisacodyl. https://reference.medscape.com/drug/dulcolax-correctol-bisacodyl-342008#91. Imechukuliwa 05.06.2022

3. NHS. Bisacodyl. https://www.nhs.uk/medicines/bisacodyl/#:.Imechukuliwa 05.06.2022

4. Kudo K, Miyazaki C, Kadoya R, Imamura T, Jitsufuchi N, Ikeda N: Laxative poisoning: toxicological analysis of bisacodyl and its metabolite in urine, serum, and stool. J Anal Toxicol. 1998 Jul-Aug;22(4):274-8.

5. Roth W, Beschke K: [Pharmacokinetics and laxative effect of bisacodyl following administration of various dosage forms]. Arzneimittelforschung. 1988 Apr;38(4):570-4.

6. Manabe N, Cremonini F, Camilleri M, Sandborn WJ, Burton DD: Effects of bisacodyl on ascending colon emptying and overall colonic transit in healthy volunteers. Aliment Pharmacol Ther. 2009 Nov 1;30(9):930-6. doi: 10.1111/j.1365-2036.2009.04118.x. Epub 2009 Aug 12.

7. Krueger D, Demir IE, Ceyhan GO, Zeller F, Schemann M: bis-(p-hydroxyphenyl)-pyridyl-2-methane (BHPM)-the active metabolite of the laxatives bisacodyl and sodium picosulfate-enhances contractility and secretion in human intestine in vitro. Neurogastroenterol Motil. 2018 Jul;30(7):e13311. doi: 10.1111/nmo.13311. Epub 2018 Feb 14.

8. Friedrich C, Richter E, Trommeshauser D, de Kruif S, van Iersel T, Mandel K, Gessner U: Absence of excretion of the active moiety of bisacodyl and sodium picosulfate into human breast milk: an open-label, parallel-group, multiple-dose study in healthy lactating women. Drug Metab Pharmacokinet. 2011;26(5):458-64. doi: 10.2133/dmpk.dmpk-11-rg-007. Epub 2011 Jun 21.

9. Ikarashi N, Baba K, Ushiki T, Kon R, Mimura A, Toda T, Ishii M, Ochiai W, Sugiyama K: The laxative effect of bisacodyl is attributable to decreased aquaporin-3 expression in the colon induced by increased PGE2 secretion from macrophages. Am J Physiol Gastrointest Liver Physiol. 2011 Nov;301(5):G887-95. doi: 10.1152/ajpgi.00286.2011. Epub 2011 Aug 25.
bottom of page