top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Agosti 2020 17:43:27

Dawa ya Amphotericin- B

Dawa ya Amphotericin- B

Amphotericin B ni dawa mojawapo ya kutibu maradhi makali ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Fungizone.


Fomu na uzito wa Amphotericin- B


Amphotericin B hupatikana katika fomu ya unga kwa ajili unaochanganywa na maji ili kuingia mwilini kwa kuchomwa sindano. Unga huu huwa kwenye vial yenye uzito wa miligramu 50mg/kwa vial


Namba Amphotericin- B inavyofanya kazi


Dawa hii hutumika kwa ajili ya wagonjwa wenye fangasi sugu na wenye upungufu wa kinga mwilini. Dawa ya Amphotericin B ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu kweney ukuta wa seli ya fangasi na kufanya ukuta wa seli kuwa na udhaifu ambapo hupelekea seli hiyo kufa


Dawa zilizo kundi moja na Amphotericin- B


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:

• Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Econazole • Flucytosine • Griseofulvin • Itraconazole • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole


Kazi ya Amphotericin- B

Hutumika kwenye matibabu ya maradhi makali yanayosababishwa na fangasi kama aspergillosis, blastomycosis, candidiasis, coccidioidomycosis, na cryptococcosis Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya Leishmaniasis Mara nyingi dawa hii huwa natumika pamoja na Flucytocine


Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Amphotericin- B


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo: • Amikacin • Cidofovir • Cyclosporine • Loversol • Neomycin PO • Streptozocin • Tacrolimus • Teicoplanin


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Amphotericin- B


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Utofauti wa Amphotericin- B na dawa zilizo kundi moja


Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni siku 15 tangia utumie dawa kunywa kwenye mwili.


Matumizi ya Amphotericin- B kwa mama mjamzito


Dawa hii ipo kwenye kundi B ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito Dawa hii hushauriwa kutumika kipindi cha ujauzito isipokuwa endapo faida zinazidi madhara yanayoweza kujitokeza


Matumizi ya Amphotericin- B kwa mama anayenyonyesha


Takwimu hazionyeshi kuwa kuna huwezekano wa hii dawa kuingiaau haiwezi kuwa kwenye maziwa ya mtoto hivyo inashauriwa itumike kwa wamama wanaonyonyesha kwa uangalifu mkubwa.


Maudhi ya Amphotericin- B


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : •Kichefuchefu •Kutapika •Maumivu ya tumbo na kichwa •Kizunguzungu •Kuharisha •Kukosa hamu ya kula •Shinikizo la damu •Kupata homa •Mwili kuwa mdhaifu


Endapo umesahau dozi ya Amphotericin- B


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ? Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1. Drugs.Amphotericin B.https://www.drugs.com/mtm/amphotericin-b.html. Imechukuliwa 8/8/2020

2. Medscape.Amphotericin B.https://reference.medscape.com/drug/amphotericin-b-conventional-amphotericin-b-deoxycholate-342582#3. Imechukuliwa 8/8/2020

3. WebMd.Amphotericin B.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-13565/amphotericin-b-injection/details. Imechukuliwa 8/8/2020

4. MedicinePlus.Amphotericin B.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682643.html. Imechukuliwa 8/8/2020

5. Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 596-601

6. Drugbank.Amphotericin B.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00681. Imechukuliwa 8/8/2020
bottom of page