Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Agosti 2020 17:50:11
Dawa ya Capsofungin
Capsofungin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya echinocandins. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Cansidas
Fomu ya dawa Capsofungin
Capsofungin hupatikana katika fomu ya unga yenye uzito kwa kila vial miligramu • 50mg • 70mg
Namna Capsofungin inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa ya Capsofungin ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa echinocandin ambayo ni sehemu muhimu ya ukuta wa seli ya fangasi ambapo seli huwa dhaifu na hupelekea kuharibika kwa ukuta wa seli ya fangasi na hatimaye kufa kwa seli.
Dawa zilizo kundi moja na Capsofungin
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
• MIcafungin • Anidulafungin
Kazi za Capsofungin
Dawa hii hutumika kwa ajili ya wagonjwa wenye fangasi sugu na wenye upungufu wa kinga mwilini.
Dawa zisizopaswa kutumika na Capsofungin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
• Cyclosporine • Eluxadoline
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Capsofungin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Utofauti wa Capsofungin na dawa zingine zilizo kundi la Echinocandins
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 9 mpaka 11 tangia utumie dawa kunywa kwenye mwili. Dawa hii hutolewa mwili kwa njia ya mkojo asilimia 41 na kwa njia ya kinyesi kwa asilimia 35
Matumizi ya Capsofungin kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito Dawa hii hushauriwa kutumika wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Capsofungin kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto ila itumike kwa wamama wajawazito kwa uangalifu.
Maudhi ya matumizi ya Capsofungin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : •Kupata vipele •Kuhisi kuungua •Maumivu ya tumbo •Kuwashwa mwili •Kichefuchefu •Kutapika •Maumivu ya tumbo na kichwa •Kizunguzungu •Kuharisha •Kukosa hamu ya kula •Kuongezeka kwa Shinikizo la damu •Kupata homa •Mwili kuwa mdhaifu
Je endapo utasahau kutumia dozi yako Capsofungin ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-