Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020, 06:14:43
Dawa ya Demeclocycline
Demeclocycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la declomycin.
Muda wa dawa kuanza kufanya kazi
Dawa hii hufanya kazi pale inaponyewa Saa 1 au masaa 2 baada ya kula Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa
Fomu ya dawa
Demeclocycline hupatikana katika mfumo wa kidonge wenye uzito wa milligramu zifuatazo:
150 mg
300 mg
Namna dawa inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini kwenye bakteria
Dawa zilizo kwenye kundi moja na Demeclocycline
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Tetracycline) na dawa hii ni ;
Choltetracycline
Oxytetracycline
Tetracycline
Doxycycline
Minocycline
Methacyxline
Rolitetracyxline
Demeclocycline hutibu nini
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa Bronchitis ya muda mrefu
Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa brucellosis
Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa Trakoma
Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa conjunctivitis
Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa kipindupindu
Utofauti wa Demeclocycline na dawa zingine za Tetracycline)
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 11 hadi 17 tangu itumike mwilini
Usitumie Demeclocycline pamoja na
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acitretin
Flibanserin
Lomitapide
Tretinoin
flibanserin
lomitapide
tretinoin
Aluminum hydroxide
Aminolevulinic acid
Amoxicillin
Ampicillin
Apalutamide
Atracurium
Avapritinib
Axitinib
Bismuth subsalicylate
Bosutinib
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Carbonyl iron
Cisatracurium
Cobimetinib
Dicloxacillin
Eliglustat
Demeclocycline isitumike kwa watu wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline
Wagonjwa wa ini
Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni
Tahadhari ya Demeclocycline
Dozi ya Demeclocycline inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo
Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8
Demeclocycline na ujauzito
Demeclocycline inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapo hairuhusiwi kutumika.
Demeclocycline kipindi cha kunyonyonyesha
Demeclocycline inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya Demeclocycline
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kutapika
Kuvimba mdomo
Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo
Je, kama umesahau dozi ya demeclocycline ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiria ufike kisha endelea na dozi kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-