Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Agosti 2020 17:58:18
Dawa ya Micafungin
Micafungin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Mycamine
Fomu ya dawa Micafungin
Micafungin hupatikana katika fomu ya unga katika vial moja. Vial moja huwa na uzito wa
50mg au
100mg
Namna Micafungin inavyofanya kazi
Dawa ya Micafungin ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kuzuia utengenezajwi wa glucan ambayo ni moja ya kiungo muhimu kwenye seli ya fangasi, Hufanya hivi kwa kuzuia kimeng’enya cha Glucan synthase kufanya kazi, ukuaji wa seli ya fangasi husimama na kisha hufa.
Dawa zilizo kundi moja na Micafungin
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Caspofungin
Micafungin
Anidulafungin
Kazi ya dawa Micafungin
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Micafungin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Micafungin kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Micafungin kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila hushauriwi itumike kwa uangalifu mkubwa.
Maudhi ya Micafungin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii nini;
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Kutapika
Kichefuchefu
Kuwashwa mwilini
Uso kuja maji
Je endapo utasahau kutumia dozi yako ya Micafungin ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa au kupaka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-