Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
2 Desemba 2020 10:50:25
Dawa ya Nitrofurantoin
Ni dawa mojawapo ya kutibu maambukizi ya bakteria na hutumika sana kwa wajawazito kutibu UTI isiyo sugu kwa kuwa imeonekana haina madhara. Dawa hii ipo katika kundi la dawa linaloitwa. Zamani ilikuwa imewekwa kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito.
Jina jingine la dawa hii
Majina mengine ya kibiashara ya dawa hii ni Furadantin, Macrobid, Macrodantin na Nitro Macro
Dawa hii hupatikana katika fomu ya
Kimiminika na
Tembe
Tembe huwa na uzito wa
Miligramu 50 hadi 100
Namna dawa inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuzuia shughuli za kimetaboliki ndani ya seli ya bakteria kwa kuzuia mzunguko wa citric acid na uzalishaji wa vinasaba vya bakteria (DNA na RNA) ya bakteria na hivyo kufanya bakteria afe
Ufyonzaji wa dawa
Dawa hii hufyonzwa na kufika kwenye damu kwa asilimia 38 hadi 44 tu. Endapo dawa itatumiwa pamoja na chakula itafyonzwa kwa kiasi kikubwa na kubaki muda mrefu Zaidi mwilini.
Namna dawa inavyotolewa mwilini
Dawa hii kabla ya kutolewa nje ya mwili huvunjwa na ini, asilimia 25-50 ya kiini cha dawa hutolewa kama ilivyo bila kuvunjwa na ini. Asilimia 90 ya dawa yote unayokunywa hutolewa kwa njia ya mkojo.
Dawa inadumu masaa mangapi mwilini?
Dawa hii ina uwezo wa kudumu kwa muda wa masaa 16.7 hadi 19.4 kwenye damu.
Maudhi ya dawa hii
Baadhi ya maudhi ya kutumia dawa hii ni;
Kichefuchefu
Kutapika
Kuvurufika kwa tumbo
Kutoa mkojo wa njano iliyokola au nyeupe iliyopauka
Kupoteza hamu ya kula
Baadhi ya madhara makubwa yaanayoweza kujitokeza endapo umetumia dozi kubwa zaidi ni;
Kushindwa kupumua
Kuchoka sana
Homa na kutetemeka
Maumivu ya kifua
Kikohozi endelevu
Ganzi. Hisia za kuchomachoma kwenye miguu
Kuvimba kwa midomo au ulimi
Harara kwenye ngozi
Aina ya bakteria wanaouliwa na dawa hii ni
Bakteria aina ya gramu positive na gramu negative
Magonjwa yanayotibiwa na dawa hii
Dawa hii hutumika kutibu magonjwa yafuatayo kwa watu wazima na watoto
Maambukizi ya bakteria kwenye kibofu cha mkojo
Maambukizi ya bakteria kwenye njia za mkojo
Kujikinga na maambukizi ya bakteria kwenye kibofu cha mkojo
Watu wasiopaswa kutumia
Watu wasiopaswa kutumia dawa hii ni wale;
Wenye figo iliyoferi au ugonjwa wa figo
Kuwa na historia ya kupata manjano
Kuwa na aleji na dawa hii
Kwa watu wanaokojoa chini ya kiwango kilicho kawaida yao
Kama upo wiki mbili au nne za mwisho katika ujauzito(yaani kipindi cha mwezi wa tisa wa ujauzito)
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa hizi
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya kipindupindu
Chanjo hai ya typhoid
Darolutamide
Lasmiditan
Pexidartinib
Pretomanid
Selinexor
Nitrofurantoin endapo itatumika na dawa zifuatazo mgonjwa anatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu sana
Acalabrutinib
Aluminum hydroxide
Apalutamide
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Bupivacaine implant
Calcium carbonate
Conjugated estrogens
Dawa ya kupaka ya Dapsone
Dawa ya kupaka ya Oxybutynin
Didanosine
Digoxin
Eluxadoline
Estradiol
Estrogens conjugated synthetic
Estropipate
Ethinylestradiol
Fostemsavir
Glecaprevir/pibrentasvir
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Mestranol
Mipomersen
Monitor closely (35)
Oxybutynin
Oxybutynin transdermal
Ponatinib
Regorafenib
Safinamide
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Sofosbuvir/velpatasvir
Stiripentol
Tafamidis
Tafamidis meglumine
Tetracaine
Trimagnesium citrate anhydrous
Matumizi ya dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipinid cha ujauzito. Kufahamu kuhusu madhara kwako au kwenye ujauzito wako wasiliana na daktari wako tafadhari
Matumizi kipindi cha ujauzito
Kama upo wiki kuanzia nne za kuelekea kipindi cha kujifungua, hupaswi kutumia dawa hii. Wasiliana na daktari wako kuhusu dawa unayopaswa kutumia kipindi hiki.
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kutumika wakati wa kunyonyesha endapo kwa mtoto amabaye ana umri Zaidi ya mwezi mmoja na hana matatizo ya damu ikiwa pamoja na ugonjwa wa G6PD. Hata hivyo Hakuna tafiti ambayo imeonuyesha kutokea kwa madhara yaliyoripotiwa kwa watoto walio kuwa kwenye kihatarishi yaani kuwa chini ya umri wa siku 8. Utumiaji wa dawa hii kwa wamama wanaonyonyesha inabaki kuwa uchaguzi wa daktari na matumizi ya dawa hii yasiwe sababu ya mama kuacha kunyonyesha mtoto.
Endapo umesahau kutumia dozi ufanyaje?
Endapo umesahau kutumia dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, usinywe endapo muda wa kunywa dozi ingine umekaribia kama utakavyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-