Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 13:00:51
Dawa ya Omoconazole
Omoconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyo katika kundi la dawa linaloitwa Imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Mikogal.
Fomu na uzito wa dawa Omoconazole
Omoconaze hupatikana pia katika fomu ya Kidonge aina ya pessary vyenye miligramu
150
300
900
Omoconazole hupatikana pia katika mfumo wa krimu wenye ujazo mbalimbali na asilimia 1 ya kiini cha dawa
Namna Omoconazole inavyofanya kazi
Dawa ya Omoconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la Imidazole, Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa homoni muhimu ya egosteroli ambayo hufanya kazi ya kutengeneza vijenzi vya ukuta wa seli.
Dawa zilizo kundi moja na Omoconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Butoconazole
Clotrimazole
Econazole
Fenticonazole
Isoconazole
Ketoconazole
Luliconazole
Oxiconazole
Sertaconazole
Sulconazole
Tioconazole
Kazi ya Omoconazole
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi kwenye ngozi
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Omoconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Tahadhari kwa watumiaji wa Omoconazole
Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa ni ni pamoja na wagonjwa wenye aleji na dawa nyingine za antifangasi
Matumizi ya Omoconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Omoconazole kwa mama nayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wajawazito
Maudhi ya Omoconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya kutumia dawa hii ni pamoja na :
Kupata vipele
Kuhisi kuungua
Maumivu ya tumbo
Kuwashwa mwili
Endapo umesahau dozi ya Omoconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-