Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Julai 2020, 19:20:57
Dawa ya Sulconazole
Sulconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Exelderm
Sulconazole hupatikana katika mfumo wa krimu yenye uzito na ujazo mbalimbali.
Namna dawa inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa hii ya Sulconazole hufanya kazi zake kwa kuharibu ukuta wa seli ya fangasi. Sulconazole na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa ergosteroli ambayo huhitajika kwa ajili ya kutengeneza ukuta wa seli ya fangasi. Egosteroli huwa muhimu sana kwenye seli ya fangasi. Kama ergosteroli haitengenezwi, seli ya fangasi hushindwa kutengeneza ukuta wake wan je na hufa.
Dawa hii ipo katika kundi moja sawa na dawa zifuatazo:
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Ciclopiro
Econazole
Fluconazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Ketoconazole
Miconazole
Naftifine hydrochloride
Nystatin
Oxiconazole nitrate
Terbinifine
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi aina ya Tinea.
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii hushauriwa kutumika endapo faida zinazidi madhara au pale ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Takwimu hazionyeshi kuwa kuna huwezekano wa hii dawa kuingia au hapana kwenye maziwa ya mama hivyo inashauriwa itumike kwa wamama wanaonyonyesha kwa huangalifu mkubwa.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na :
Kuwashwa mwilini
Kuhisi kuungua mwilini
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo umesahau kutumia dozi yako, paka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-