Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
25 Juni 2020, 18:49:20
Ethacrynic Acid
Ni dawa moja wapo ya kutibu kuvimba kwa sehemu za mwili kama miguu. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa za Loop Diuretics nahuwa maarafu kwa jina la Edecrin
Rangi ya Ethacrynic Acid
Rangi ya dawa huweza kuwa nyeupe ,lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza
Matumizi na chakula
Ethacrynic Acid haina madhara inapotumika pamoja na chakula
Fomu na uzito wa Ethacrynic
Ethacrynic acid hupatikana katika mfumo wa kidonge cha uzito wa Milligram 25 pia hupatikana katika mfumo wa powder kwa ajili ya sindano katika uzito wa Miligramu 50
Ufanyaji kazi
Ethacrynic Acid hufanya kazi kwa kuzuia ufyozwaji wa maji kwenye mirija ya figo na hii humpelekea mtu kukojoa mara kwa mara
Ufyozwaji wa maji unapozuiwa hurusu maji mengi kwenye mwilini kupungua na hivyo kupunguza miguu kuvimba kwa wagonjwa wa moyo na wenye shida ya ini na figo
Dawa kundi moja na Ethacrynic Acid
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Bumetadine (Bumex)
Furosemide (Lasix)
Torsemide (Demadex)
Ethacrynic Acid hutibu nini?
Hutumika kutibu hali ya kuvimba kwa sehemu za mwili kama miguu na uso ambayo hali hii huweza kuwatokea wagonjwa walioferi moyo na wagonjwa wa ini mfano ini kusinyaa, wagonjwa wa figo sindromu ya nephrotiki.
Dawa zisizopaswa kutumiaka na Ethacrynic Acid
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Amikacin
Baricitinib
Furosemide
Gentamicin
Lofexidine
Neomycin
Paromomycin
Squill
Streptomycin
Tobramycin
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye aleji na dawa hii na mgonjwa mwenye shida ya kukojoa pamoja na watoto chini ya siku 28
Tahadhari kwa watumiaji wa Ethacrynic Acid
Huweza kupelekea hatari ya kupoteza madini muhimu mwilini na yapo madhara mengi ya kupoteza madini hayo mfano kuogezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu, shinikizo la damu kuwa la chini, kupungukiwa kwa madini ya potasiamu na sodiamu na kuishiwa maji mwilini.
Endapo itatumika kwa mgonjwa mwenye tatizo la kupitisha mkojo vema anapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu
Matumizi ya Ethacrynic Acid kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha
Maudhi ya Ethacrynic Acid
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na;
Kuongezeka kwa kiwango cha uriki aside kwenye mkojo
Gauti
Shinikizo la damu kuwa chini
Kuwa na upungufu wa madini ya Potasiamu
Kuwa na upungufu wa madinimwilini
Sukari kuwa juu
Mwili kuwa na mafuta sana
Sumu sikioni
Mlio kwenye sikio
Misuli kukaza
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kutapika
Kukosa hamu ya kula
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dawa anapaswa kutumia pindi anapokumbuka, endapo muda wa dozi umekaribia sana basin i vema kuruka dozi uliyosahauna endelea kwa muda ule ule kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-