Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Aprili 2020, 07:58:49
Glyclopyramide
Glycopyramide ni dawa inayotumika kuthibiti kupanda kwa kiwango cha sukari wkenye damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya Pili. Dawa hii ipo katika kundi la dawa linaloitwa sulfonylurea kizazi cha pili na huweza kusababisha mgonjwa akakojoa mara kwa mara.
Ukilinganisha na dawa zingine katika kundi hili, glycopyramide inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi huku ikiwa na madhara kidogo mwilini.
Majina ya kibiashara
Jina la kibiashara la Glyclopyramide ni Deamelin
Fomula ya kikemikali
Fomu ya kikemikali ya Glyclopyramide ni C11H14ClN3O3S
Jina la kisayansi (IUPAC)
Jina la kisayansi la Glyclopyramide ni 1-(4-chlorophenyl)sulfonyl-3-pyrrolidin-1-ylurea
Namna ya kutumia Glyclopyramide
Meza kama ulivyo elekezwa na daktari wako.
Ufanyaji kazi wa Glyclopyramide
Inachochea seli beta za kongosho kuzalisha homoni insulin ambayo ndiyo hushusha sukari kwenye damu.
Inapunguza kasi ya ini kutengeneza sukari
Inaongeza uwezo wa ufanisi wa vipokezi vya homoni insulin kwenye seli za mwili hivyo homoni hii kufanya kazi vizuri.
Umetaboli wa Glyclopyramide
Hufika kwenye damu baada ya kufyonzwa kutoka kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondoa sumu.
Sehumu kubwa ya takamwili za mabaki ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo.
Muingiliano wa Glyclopyramide na dawa zingine
Dawa zifuatazo zinaweza kuongeza ufanisi wa glycopyramide;
Chloramphenicol
Clofibrate
Fluconazole
Methyldopa
Isocarboxazid
(Marplan)
Phenelzine (Nardil)
Tranylcypromine (Parnate).
Choline salicylate
Diflunisal
Magnesium salicylate
Salsalate
Sodium salicylate
Sodium thiosalicylate
Sulfamethizole
Sulfamethoxazole
Sulfasalazine
Sulfisoxazole
Trimethoprim
Trimethoprim–sulfamethoxazole
Trisulfapyrimidine
Trovafloxacin
Dawa zifuatazo zinaweza kupunguza ufanisi wa glycopyramide;
Vidonge vya uzazi wa mpango
Amlodipine
Bepridil
Diltiazem
Nicardipine
Nifedipine
Verapamil
Betamethasone
Budesonide
Dexamethasone
Dexone,
Hydrocortisone
Sodium phosphate
Isoniazid
Nani asuyepasw akutumia Glyclopyramide
Marufuku kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na kemikali zenye salfa.
Wagonjwa wa sukari inayotibika kwa insulini pekee (sukari aina ya kwanza).
Wagonjwa ambao figo zinashindwa kufanya kazi.
Maudhi madogo ya Glyclopyramide
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Kichefuchefu
Kuwashwa ngozi
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Madhara makubwa ya Glyclopyramide
Kiwango cha sukari kwenye damu kushuka kupita kiasi
Kupoteza fahamu
Mzio mkali wa sindromu ya Steven Johnson
Ini kushindwa kufanya kazi
Degedege.
Matumizi ya Glyclopyramide wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Kama ikitumiwa wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa mtoto kuna hatari ya mtoto kuzaliwa na kiwango kidogo cha sukari kwenye damu, kushindwa kupumua na kupitiliza muda wa kuzaliwa.Kama ililazimu mama kutumia dawa hii basi mama anapaswa kuacha kuitumua wiki 2 kabla ya siku ya matarajio ya kujifungua.
Pia ni vizuri kuacha kutumia wakati wa kunyonyesha, na ikibidi kutumia basi mtoto anaenyonya atawekwa kwenye uangalizi wa karibu kwa kuangalilia dalili kama vile kuwa wa blue mdomoni viganja na miguu, kulala kupita kiasi, kushindwa au kunyonya kwa udhahifu na degedege.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:33:56
Rejea za mada hii:-